Mimi ni baharia mstaafu, nilikuwa baharia zaidi yake, Nakumbuka kipindi ujana umekolea moto watu wananiona napotea hata hawanistui, marafiki wananisifia eti sukari ya warembo kumbe ndo napotea hivyo, wengine wakawa wananikuwadia totoz nagonga kweli kweli najiona kidume kumbe kwisha habari yangu, ikafika kipindi nikitongoza dem hakatai hata awe mkali vipi kumbe mapepo ya uzinzi yananisaidia, nikazidi kupotea, nikafika level ya arosto nikikosa dem navurugwa usingizi hauji, nikajua saiti zote za porn, nikimuona mdada mzuri lazima nichukue namba baadae nikawa siwasevu maana phone book ilijaa, Nilikuja kustuka nimepoteza miaka 15 kwenye zinaa, hakuna nilichopata cha maana ila nilichopoteza ni kikubwa namwomba Mungu anikumbuke anifidie, jifunze kwangu achana na ubaharia hauta kulipa