Ubishi Tu na kushupaza misuli ya shingo ilihali ukweli unaujua.
Jamaa yupo sahihi unampinga bure ukizima umezima namaanisha ukifa umekufa suala hilo hua halinaga mjadala when you are you are gone tukishapiga dua zetu tunakuzika kisha tunakusahau yaan kaburi lako linaweza likawa hata halifagiliwi na mtu, mengine tunaishia kutishana tu hapa hapa duniani hakuna aliefika uko akarudi kuja kutupa report nini kilichopo uko,
Amini kwamba hakuna anaejua alikotoka na hakuna anaejua anakoenda tupo hapa duniani tunanunua muda tu muda wako ukiisha lazima uende, ndio maana ukiumwa unajipambania upone usife mapema unajipambania unanunua muda wa kuishi duniani kila inapoitwa leo, ukikosa pesa za matibabu au ugonjwa ukigoma kutibika ndio baasi you're gone for real na ukishaenda unabadirishwa na jina hautaitwa tena James au Peter jina lako litakua kama sio hayati basi utaitwa marehemu,
Imani ikizidi sana nayo ni
mbaya inakua ni Imani potofu sometimes inabidi tujifunze ku-balance haya masuala tusitishane kupitiliza, nobody knows what's coming next in another chapter, wote tumepigwa upofu kwa hio tusijitie ujuaji sana kwenye baadhi ya mambo tuishi kwa kiasi maana muda hauna mwenyewe wote tutaondoka ila huu muda utaendelea kuwepo,
Sisi kazi yetu ni moja tu hapa duniani kununua muda ili tuishi ndio maana tunafanya kazi ili tule usipofanya kazi kula yako itakua ya taaabu na kula yako ikiwa ya taaabu maradhi yatabisha hodi na maradhi yakibisha hodi muda wako wa kuwepo hapa duniani ndivyo unavyozidi kupungua
Haya mengine ya kujamiiana nà wanawake kwa wanaume, sio jambo baya na wala halina tatizo lolote zaidi zaidi baadhi ya watu wamekua na Imani zao binafsi ni za kwao wanaamini katika kile wanachokiamini kwamba kufanya Jambo fulani basi ni laana au kufuru kwenye ulimwengu wa nafsi na roho ila all in all yote yapo ndani ya muda, muda ndio unao-ongea haijalishi unafanya nini na wapi ila ukiuchezea muda vibaya utaku-cost
Mfano:
Wewe hujawahi kufika Mwanza alafu unaanza kunieleza kuhusu Mwanza, nitakuelewaje?
Yaan wewe hujawahi kufika Dar alafu unajifanya unaijua Buguruni kuliko wanavyoijua watu wa Dar?
Namaanisha mtu unapozungumzia kuhusu masuala ya rohoni au masuala ya nafsi, nikikuhoji je wewe umewahi kufika uko zilipo hizo nafsi na roho kwenye huo ulimwengu umewahi kufika wewe?
Je! wewe umewahi kufika uko hadi unakua msemaji wa ulimwengu wa uko hadi unafika hatua ya unazisemea nafsi na roho?
Utanijibu nini?
Km hujaelewa hapo basi huwezi kuelewa milele
Muuuda tumia Muda wako vizuri ukienda umeenda asikuongopee mtu sijui utaona nini sijui itakuaje ukienda utakuaje hakunaga hizo habari
Umekuja ukiwa mikono mitupu na siku ukilala utalala mikono mitupu acha kuwatisha watu