Basi bwana! Haya ya nyuma yalichunguzwa na watu wakawajibika. Kwanini haya hayachunguzwi? Kwanini CCTV zilitolewa baada ya Lisu kupigwa risasi.... ukisema ushahidi, muuaji huwa anatumia kisingizio cha leta ushahidi kukwepa adhabu!Sina hakika unataka kusema nini? Mauaji ya sasa serikali inahusika vipi...leta ushahidi hapa kuhusu namna serikali inavyohusika na mauaji...Je, wale vijana wa madini hukumbuki kuwa polisi walidaiwa kuhusika na ambapo senior police officer alifikishwa mahakamani? Je, mauaji ya operesheni fulani iliyofanyika huko Shinyanga na watu kadhaa wakateswa na kufa na hata Waziri wa mambo ya ndani wakati huo kujiuzulu (ambapo baadaye alikuja rais ) je serikali haikuhusika hapo? Tuwe wakweli katika mambo haya....ni mauaji gani yamefanyika katika awamu hii ya JPM na kama yapo ni ushahidi upi unathibitisha kuwa serikali inahusika? Ni demokrasia gani hiyo imeminywa?
Kweli Magereza walikosa gari la kuwaleta Mbowe mahakamani? Kuwa mkweli na utakuwa huru. Nina uhakika wewe una madaraka serikalini, rekebisha haya mambo.... demokrasia ya kutoa maoni, kukosoa haipo, jaribu kusema rais hana mamlaka ya kutumia pesa kujenga uwanja chatobila idhini ya bunge kama hutatoweka leo leo... mambo kama hayo! 1954, wewe ni mtumzima sana, una madaraka, rekebisha pale watu wanapopalalamikia! Maaskofu ni wapenzi wazuri wa JPM, lkn wameona kasoro wamejitenga! Nao ni hopeless, ?