Siku ikitokea tamthilia kali na nzuri kuliko Prison Break naomba mnishtue

Siku ikitokea tamthilia kali na nzuri kuliko Prison Break naomba mnishtue

Kinumbo

JF-Expert Member
Joined
Dec 8, 2019
Posts
3,039
Reaction score
5,560
Jamboo!

Wakuu kama kichwa cha mada kinavyo jieleza hapo juu naomba hiyo ikitokea mniambie nitakuwa hapa panapo majaliwa. Binafsi ni mpenzi wa kutizama na kufuatilia filamu na tamthilia mbali mbali, pale nipatapo muda wa ziada basi huwa naburudika kwa kutizama filamu ama tamthilia.

Mpaka sasa nimetizama filamu na tamthilia nyingi tu, katika zote kuna tamthilia iliyo pewa jina la Prison Break nathubutu kusema hii ndio tamthilia iliyo kuwa bora n nzuri zaidi kutizama mpaka sasa. Nimetizama tamthilia kama Blacklist, Game of Throne, Breaking Bad, Money Heist, Viking, 24 Hours, Iris, The Wire, Twin Peaks, Walking Dead, nakadhalika nakadhalika.

Katika tamthilia zote nilizo tizama kiukweli tamthilia ya Prison Break ni nzuri sana na sijaona kali kuliko hiyo. Uzuri wake unachangiwa stori yake, wahusika kuuvaa huusika vile inavyo takikana pamoja na mazingira. Stori ya tamthilia ya Prison Break ni nzuri sana kuanzia msimu wa kwanza mpaka msimu wa tano stori yake imepangwa kwa mtiririko mzuri na wenye kuvutia, hii inakufanya kila episode inapo isha utamani kujua kilicho fuata. Upande wa Mazingira hapa pia waongozaji walipatia sana, nilicho penda ni wahusika kucheza kwenye magereza halisi kabisa. Gereza la Fox River na Sona wahusika walicheza ndani ya magereza halisi na wala sio studio, hiyo ilivutia zaidi.

Kwenye kipengele cha wahusika hapa ndio nilipenda zaidi, hii ndio tamthilia niliyo shuhudia wahusika wameuzaa uhusika vile ipasavyo kiasi kwamba unahisi ni kweli. Muhusika kama Fernando Sucre nilipenda sana alivyo uvaa uhusika hasa kwenye mapenzi kwa mpenzi wake ilivutia sana, muhusika Benjamin Miles ama C Note kama alivyo penda kuitwa zile scene za mapenzi ya dhati kwa binti yake kwa kweli zina sisimua na kufurahisha unahisi kama kweli kumbe maigizo. Askari magereza Brad Bellick huyu jamaa alikuwa na ongea fulani hivi ya kikauzu, nilikuwa nacheka sana nikimuona akiongea. Aliutendea haki u askari magereza alipo kuwa katika gerezaa Fox River. Agent Mohone aisee huyu mwamba alionyesha kipaji kikubwa sana kwenye msimu wa pili na wa tatu, msimu wa tatu kule Sona alicheza vizuri sanaaaaa. Kuna mwamba T Bag huyu drama zake zilikuwa nyingi sana, bila kuwasahau wahusika wakuu Michael Scofield na Lincoln Burrows hawa wawili walitisha sana.

Tamthilia ya Prison Break ndio nilio itizama mara tatu zaidi kwa kuirudia rudia haichoshi wa hai boi, bonge moja la tamthilia. Sasa kama kuna kali zaidi ya hiyo hebu naomba uniambie nikaitizame.
 
Kuna scene baada ya Scofield kukataa kusema namna amepata jeraha mgongoni baada ya kuungua ilihitajika pesa ya kuhonga kwa askari ili wapate chumba alicho kuwa akilala Scofield maana walisikia chumba anataka kupewa mtu mwingine tofauti na wao wanao taka kutoroka. C Note ikabidi aende kwa manigga wenzake kuomba pesa matokeo yake alidudwa mbovu maana wale jamaa walihisi ana wageuka manigga wenzake na kujiunga na ma white, pale gerezani kulikuwa na matabaka ya wafungwa weusi na weupe.

C Note anarudi kutoka aliko pigwa kipigo kizito ana wakuta D Cooper na T Bag wakipata chakula, T Bag kumuona alivyo dundwa akamwambia "look like a Bank of Africa wasn't allowing any withdrawals". Hahahaa T Bag alikuwa mnyama sana, hiyo series T Bag aliinogesha sana.
Kwanini umemuelezea kidogo T-bag umeniudhi. [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] Huyu Snitch sio wakumuamini kamwe
 
Nilipenda walivyoihusisha na story ya Dany Cooper (D cooper) huyu mwamba ana story yake ya kweli kabisa, aliiba pesa nyingi Marekani na hajawahi kamatwa mpaka Leo....ndio hiyo story naikuta kwa akina Scofield et Ile pesa kina Brady, T bagwell na akina Scofield walikuwa wanagombania et Cooper aliwapa ramani 😅😂😂😂😂😂okay ila far more MJUE ilo goma ni la 2005 nadhani na limewahi rushwa kama ilivyokuwa inarushwa Isidingo ITV...

ALAFU juzi kati nikiangalia movie moja Inaitwa "EMPIRE" season 2, Bwana weeeeeh!! sinamuona "Alexander Mahonney" daaah huyu mwamba, ila hakutisha sana maake eti alikuwa muwakilishi wa LGBTQ🤮🤢 afu kazeeka mbaya! Enewei, GOAT ni movie kali, BREAKING BAD is my next kick after PB, alafu MERLIN, LEGENDS OF THE SEEKER...sema ubaya wa hizi ngoma hawajuagi namna ya kuwa na mwisho wa kumridhisha mtazamaji..

One love men...naendelea na EMPIRE ila umeanza kubore.
 
Tazama LAW OF LOVE kupitia ITV superbrand hutajuta. Humo utakutana na mzee Alonso, Carlos, Benjamin, Olvia, Hellen, Luan, Jaji Marufo, Ricardo, Leonardo n.k
 
😂😂😂😂Ile character yule chizi aliweza halafu Wala Hana time sasa
Hana habari na ana zali michongo huwa inamkuta juu kwa juu tu, kama alivyojua dili la kutoroka alikuwa anataka kumbandua askari 😂😂😂😂 ila t bag hapana, ye mwenyewe alikuwa anasema yeye ni last line ya corrupt breed, there shall be no more of them after he dies 🙌🙌🙌🙌🙌
 
Back
Top Bottom