Siku ikitokea tamthilia kali na nzuri kuliko Prison Break naomba mnishtue

Siku ikitokea tamthilia kali na nzuri kuliko Prison Break naomba mnishtue

Power kuna mwamba wakuitwa Ghost na mpambe wake Tony mixa wife Tasha.... Hi familia inakuja kuongezwa na mchepuko askari jina nimemsahau. Kufa kwa ghost ndio ukawa mwisho wa kuifatilia izo bookbook
 
Jamboo!

Wakuu kama kichwa cha mada kinavyo jieleza hapo juu naomba hiyo ikitokea mniambie nitakuwa hapa panapo majaliwa. Binafsi ni mpenzi wa kutizama na kufuatilia filamu na tamthilia mbali mbali, pale nipatapo muda wa ziada basi huwa naburudika kwa kutizama filamu ama tamthilia.

Mpaka sasa nimetizama filamu na tamthilia nyingi tu, katika zote kuna tamthilia iliyo pewa jina la Prison Break nathubutu kusema hii ndio tamthilia iliyo kuwa bora n nzuri zaidi kutizama mpaka sasa. Nimetizama tamthilia kama Blacklist, Game of Throne, Breaking Bad, Money Heist, Viking, 24 Hours, Iris, The Wire, Twin Peaks, Walking Dead, nakadhalika nakadhalika.

Katika tamthilia zote nilizo tizama kiukweli tamthilia ya Prison Break ni nzuri sana na sijaona kali kuliko hiyo. Uzuri wake unachangiwa stori yake, wahusika kuuvaa huusika vile inavyo takikana pamoja na mazingira. Stori ya tamthilia ya Prison Break ni nzuri sana kuanzia msimu wa kwanza mpaka msimu wa tano stori yake imepangwa kwa mtiririko mzuri na wenye kuvutia, hii inakufanya kila episode inapo isha utamani kujua kilicho fuata. Upande wa Mazingira hapa pia waongozaji walipatia sana, nilicho penda ni wahusika kucheza kwenye magereza halisi kabisa. Gereza la Fox River na Sona wahusika walicheza ndani ya magereza halisi na wala sio studio, hiyo ilivutia zaidi.

Kwenye kipengele cha wahusika hapa ndio nilipenda zaidi, hii ndio tamthilia niliyo shuhudia wahusika wameuzaa uhusika vile ipasavyo kiasi kwamba unahisi ni kweli. Muhusika kama Fernando Sucre nilipenda sana alivyo uvaa uhusika hasa kwenye mapenzi kwa mpenzi wake ilivutia sana, muhusika Benjamin Miles ama C Note kama alivyo penda kuitwa zile scene za mapenzi ya dhati kwa binti yake kwa kweli zina sisimua na kufurahisha unahisi kama kweli kumbe maigizo. Askari magereza Brad Bellick huyu jamaa alikuwa na ongea fulani hivi ya kikauzu, nilikuwa nacheka sana nikimuona akiongea. Aliutendea haki u askari magereza alipo kuwa katika gerezaa Fox River. Agent Mohone aisee huyu mwamba alionyesha kipaji kikubwa sana kwenye msimu wa pili na wa tatu, msimu wa tatu kule Sona alicheza vizuri sanaaaaa. Kuna mwamba T Bag huyu drama zake zilikuwa nyingi sana, bila kuwasahau wahusika wakuu Michael Scofield na Lincoln Burrows hawa wawili walitisha sana.

Tamthilia ya Prison Break ndio nilio itizama mara tatu zaidi kwa kuirudia rudia haichoshi wa hai boi, bonge moja la tamthilia. Sasa kama kuna kali zaidi ya hiyo hebu naomba uniambie nikaitizame.
Sona sio gereza aisee, ila nilivyojua Wenthwoth Miller ni bwabwa palepale mzuka ulikata.
 
Money Heist kama walitaka kuja hivi ila walipoingiza ujinga wao kwishnei.
 
T Bag alikuwa na bahati sana ama ni muongozaji alitaka iwe hivyo. Katika wote walio toroka kule Fox River ni yeye pekee alikuwa akipita popote mtaani bila kushukiwa na raia. Lile bifu lake na Abruzzi lilikuwa ni burudani sana muda wote wanawindana na hawaaminiani kabisa.
Nilipenda walivyoihusisha na story ya Dany Cooper (D cooper) huyu mwamba ana story yake ya kweli kabisa, aliiba pesa nyingi Marekani na hajawahi kamatwa mpaka Leo....ndio hiyo story naikuta kwa akina Scofield et Ile pesa kina Brady, T bagwell na akina Scofield walikuwa wanagombania et Cooper aliwapa ramani [emoji28][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]okay ila far more MJUE ilo goma ni la 2005 nadhani na limewahi rushwa kama ilivyokuwa inarushwa Isidingo ITV...

ALAFU juzi kati nikiangalia movie moja Inaitwa "EMPIRE" season 2, Bwana weeeeeh!! sinamuona "Alexander Mahonney" daaah huyu mwamba, ila hakutisha sana maake eti alikuwa muwakilishi wa LGBTQ[emoji2961][emoji1785] afu kazeeka mbaya! Enewei, GOAT ni movie kali, BREAKING BAD is my next kick after PB, alafu MERLIN, LEGENDS OF THE SEEKER...sema ubaya wa hizi ngoma hawajuagi namna ya kuwa na mwisho wa kumridhisha mtazamaji..

One love men...naendelea na EMPIRE ila umeanza kubore.
 
Jamboo!

Wakuu kama kichwa cha mada kinavyo jieleza hapo juu naomba hiyo ikitokea mniambie nitakuwa hapa panapo majaliwa. Binafsi ni mpenzi wa kutizama na kufuatilia filamu na tamthilia mbali mbali, pale nipatapo muda wa ziada basi huwa naburudika kwa kutizama filamu ama tamthilia.

Mpaka sasa nimetizama filamu na tamthilia nyingi tu, katika zote kuna tamthilia iliyo pewa jina la Prison Break nathubutu kusema hii ndio tamthilia iliyo kuwa bora n nzuri zaidi kutizama mpaka sasa. Nimetizama tamthilia kama Blacklist, Game of Throne, Breaking Bad, Money Heist, Viking, 24 Hours, Iris, The Wire, Twin Peaks, Walking Dead, nakadhalika nakadhalika.

Katika tamthilia zote nilizo tizama kiukweli tamthilia ya Prison Break ni nzuri sana na sijaona kali kuliko hiyo. Uzuri wake unachangiwa stori yake, wahusika kuuvaa huusika vile inavyo takikana pamoja na mazingira. Stori ya tamthilia ya Prison Break ni nzuri sana kuanzia msimu wa kwanza mpaka msimu wa tano stori yake imepangwa kwa mtiririko mzuri na wenye kuvutia, hii inakufanya kila episode inapo isha utamani kujua kilicho fuata. Upande wa Mazingira hapa pia waongozaji walipatia sana, nilicho penda ni wahusika kucheza kwenye magereza halisi kabisa. Gereza la Fox River na Sona wahusika walicheza ndani ya magereza halisi na wala sio studio, hiyo ilivutia zaidi.

Kwenye kipengele cha wahusika hapa ndio nilipenda zaidi, hii ndio tamthilia niliyo shuhudia wahusika wameuzaa uhusika vile ipasavyo kiasi kwamba unahisi ni kweli. Muhusika kama Fernando Sucre nilipenda sana alivyo uvaa uhusika hasa kwenye mapenzi kwa mpenzi wake ilivutia sana, muhusika Benjamin Miles ama C Note kama alivyo penda kuitwa zile scene za mapenzi ya dhati kwa binti yake kwa kweli zina sisimua na kufurahisha unahisi kama kweli kumbe maigizo. Askari magereza Brad Bellick huyu jamaa alikuwa na ongea fulani hivi ya kikauzu, nilikuwa nacheka sana nikimuona akiongea. Aliutendea haki u askari magereza alipo kuwa katika gerezaa Fox River. Agent Mohone aisee huyu mwamba alionyesha kipaji kikubwa sana kwenye msimu wa pili na wa tatu, msimu wa tatu kule Sona alicheza vizuri sanaaaaa. Kuna mwamba T Bag huyu drama zake zilikuwa nyingi sana, bila kuwasahau wahusika wakuu Michael Scofield na Lincoln Burrows hawa wawili walitisha sana.

Tamthilia ya Prison Break ndio nilio itizama mara tatu zaidi kwa kuirudia rudia haichoshi wa hai boi, bonge moja la tamthilia. Sasa kama kuna kali zaidi ya hiyo hebu naomba uniambie nikaitizame.
Mimi tangu imalizike Isidingo sijawahi kuangalia hizo tamthilia.Isidingo ndiyo niliona pekee ilikuwa na uhalisia.Maana kama ni vikao vya mahakama wanafanya kabisa kimahakama,kama ni usaili wa kuwapata wafanyakazi wanafanya kiuhalisia,kama ni vikao vya bodi za kampuni vinafanyika kabisa na kuna jambo unajifunza ukilinganisha na sheria zetu na kanuni za kufanya hayo mambo nk.
 
Msimu wa kwanza mpaka wa tatu Bellick alicheza kwa ufanisi sana. Ana kwambia ameanza kazi hapo Fox River akiwa na miaka 18, baada ya Scofield na genge lake kutoroka ana achishwa kazi jamaa analia sana anadai maisha yake ni Uaskari gereza akiwa na maana hiyo ndio kazi pekee anaweza fanya kwa ufanisi.

Baadae katika pilikapilika za kutafuta ile dollar 5M kinatokea kifo cha rafiki yake ambaye walikuwa pamoja katika kusaka hizo pesa, anajichanganya pale anapo ulizwa swali na muendesha mashitaka kama ana mfahamu anajibu ndio na kudai ni rafiki yake. Kesi inapelekwa mahakamani na hukumu inatoka kutumikia adhabu akiwa gerezani, kinacho burudisha na kufundisha hapa alifungwa gereza la mbali ikabidi aombe afungwe gereza la karibu ili awe ana muona mama yake kwa karibu. Ikabidi apelekwe Fox River kule alikuwa askari magereza kabla ya hapo, akarudi kama mfungwa, baadae alikuja kutoka baada ya kupewa kazi na agent Mahone. Ila Bellick vile vituko vyake na ukauzu kule Fox River ni burudani tosha.
PB hainaga mpinzani niko naiangalia hapa Bellick anamwambia T bag kuwa uzao wake ni babake alimbaka dadake ndio yeye akazaliwa, yan mtu na kakake walitiana mimba ndio t bag akatokea [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Akianza ile staili yake ya kulamba lips kwa kutoa ulimi nje ujue kuna jambo anaenda kufanya [emoji23]
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Ile character yule chizi aliweza halafu Wala Hana time sasa
 
Mkuu muhusika alie cheza kwenye PB ni Michael Scofield na wala sio Wentworth Miller. Ndio maana kwenye PB Scofield alikuwa na mpenzi wake Sarah, tunafuatilia tamthilia ya Prison Break na sio maisha binafsi ya Wentworth Miller. Hayo mengine atajua yeye na maisha yake huko.
Sona sio gereza aisee, ila nilivyojua Wenthwoth Miller ni bwabwa palepale mzuka ulikata.
 
Kwanini umemuelezea kidogo T-bag umeniudhi. 😂😂😂😂 Huyu Snitch sio wakumuamini kamwe
Bagwel alikuwa mnyamaa 🤣🤣. Nilipenda transformation ya Belick from mamaz to a fugitive
 
Nipo nairudia hii series itoshe kusema uyu jamaa Lincoln na masikio yake alikua mkuda sana ni pimbi uyu
 
Nipo nairudia hii series itoshe kusema uyu jamaa Lincoln na masikio yake alikua mkuda sana ni pimbi uyu
Sema ana huruma sana jamaa. Basi tu alikimbia umande😂
 
Back
Top Bottom