Kinyungu
JF-Expert Member
- Apr 6, 2008
- 19,484
- 38,416
Leo ni kumbukizi ya siku ya Uhuru wa nchi ya Zanzibar.
Mnamo tarehe 10 Disemba 1963 nchi hiyo ya Zanzibar ilipata uhuru wake toka kwa wakoloni wa Uingereza ambao walikuwa wameitawala nchi hiyo kwa takriban miaka 73 (tokea 1890). Mohamed Shamte alikuwa Waziri Mkuu wa Zanzibar huru akiongoza serikali huku Sultan akiwa Jamshid bin Abdullah Al Busaidi.
Hata hivyo serikali ya Bw. Shamte haikudumu muda mrefu kwani siku 33 baadae yaani 12 Januari 1964 yalitokea mapinduzi yakiongozwa na Field Marshall John Okello toka Uganda na kufanikiwa kuipindua serikali hiyo na Shamte na Sultan akakimbilia Uingereza.
Tunawatakia Wazanzibar wote heri na fanaka katika siku hii ya kumbukizi ya uhuru wao.
View: https://x.com/HilmiHilal88/status/1866352767360553005?t=vQrLXB_mZhEJVnmMtnS0vg&s=19