Siku kama ya leo, Mwaka...

Siku kama ya leo, Mwaka...

siku kama ya leo mwaka 1954 timu ya Taifa ya soka ya Brazil waliamua kuanza kuvaa jezi za njano.

itakumbukwa kabla ya hapo Brazil walikuwa wanavaa jezi nyeupe juu na chini.
 
siku kama ya leo Shinji Kagawa mchezaji wa kimataifa toka Japan anatimiza umri wa miaka 27.
 
Farouk, mfalme wa mwisho wa Egypt alifariki siku kama ya leo akiwa na umri wa miaka 45 tu.

hii ilikuwa mwaka 1965
 
siku kama ya leo mwaka 1950 wabelgiji walipiga kura na kufanikiwa kuiangusha serikali.

adhma yao ilikuwa ni kurudi kutawaliwa na Mfalme Leopard wa tatu.
adhma hio ilifanikiwa hatimae.
 
huko New Jersey nchini marekani, tarehe kama ya leo alizaliwa mwanamuziki wa Rap, Muigizaji na pia mchekeshaji, hapa namzungumzia Queen Latifah.

hii ilikuwa ni mwaka 1970.
Queen Latifa atakumbukwa kwa kusimama imara kwenye movie ya Set it Off na pia anatakamba kwa sasa katika kipindi cha Queen Latifah talk show.

happy birthday Mama
 
siku kama ya leo mwaka 1978 hapo mjini Bujumbula alizaliwa Mwanasoka Suleiman Ndikumana...

Na nchini Kenya akazaliwa Denis Odhiambo kutoka katika viunga vya wajaluo nchini humo.

heshima kwenu wakuu
 
siku kama ya leo mwaka 2005 mwamuziki 50 Cent anafanikiwa kuwa msanii wa kwanza kuwa na nyimbo 3 ktk Top 5 nchini Marekani.

nyimbo hizo ni 'Candy shop iliokamata namba 1, na kisha 'How We Do alioshirkishwa na the Game wa kundi waliokuwa wote yani G-Unit llkukamata namba 4 na Disco Inferno' iliobamba namba 5.
 
siku kama ya leo yapata miaka 60 iliopita muigizaji Bruce Wills
 
siku kama ya leo mwaka uliopita, James Harden kinara wa Houston Rockets anaifungia timu yake jumla ya pointi 50 katika ushndi wa 118-108 dhidi ya Denver Nuggets.

itakumbukwa Harden alipanda kucheza ligi ya NBA mwaka mmoja na Bwana Hashim Thabeet....dah
 
mwaka 1977
The Golden State Warriors wanawafunga
Indiana Pacers jumla ya pointi 150 dhidi ya 91.

kibano hicho kinashikilia rekodi namba 6 katika vibano vikubwa katika ligi ya NBA.
 
1458419934126.jpg
siku kama ya leo alizaliwa bun b
 
March 20, mwaka 1984 huko katika viunga vya
Fuenlabrada nchini Spain alizaliwa mshambuliaji ambae baadae alikuja fahamika kama El Niño.

Fernando Torres jina alilopewa na wazazi wake, alikuja kuwa mchezaji wa pekee kushinda mataji ya Champions League, Europa League, World Cup na European League championships.

alianza kutamba na Atretico Madrid, na badae akajiunga na Liverpool tokea mwaka 2007 hadi 2011 alipohamia Chelsea.
katika kukamilisha kipaji chake kama ambayo nyota wengine hufanya, Torres alihamia klabu yenye mafanikio zaidi Ulimwenuni yaani AC amilan.
Torres alitanabaisha kuwa kwa yeye kujiunga na Milan ilikuwa ni kukamilisha utukufu wake kwa wapenzi wa soka.

Historia yake inasema kuwa Torres alipokuwa mdogo aliimudu nafasi ya golikipa, na alijiunga na timu ya watoto ya Atretico mwaka 1995, kabla ya kuruhusiwa kujiunga na kikosi cha kwanza mwaka 2001 hapa sasa akiwa kama mshambuliaji.
aliifungia Atretico magoli 75 katika mechi 174 za La Liga.
akiwa bwana mdogo tu pale Atretico alifanikiwa kukivaa kitambaa cha unahodha na na kuwaongoza wachezaji wenzie waliokuwa wamemzidi umri na miongoni mwao alikuwa Diego Sumeone ambae kwa sasa anamfundisha hapohapo Atretico.

alipokuwa Liverpool alifanikiwa kuwa mchezaji wa kwanza kufunga magoli zaidi ya 20 kwa msimu tangu mwaka 1996. pia akawa mchezaji wa kwanza kufikisha magoli 50 kwa kipindi kifupi katika historia ya Liverpool.
 
siku kama ya leo nchi ya Tunisia ilijitwalia uhuru wake toka kwa koloni lao yaani France.

hii ilifuatia miongo kadhaa ya mahangaiko na mataabiko.
 
'Siku kama ya leo' ni kwa ajili ya wazungu tu? Naona lots of wazungu info na kdg waafrika.

Weka na za nzengo yetu ya Tz mkuu
 
Blake Griffin nyota wa NBA ambae ameshapata kushinda tuzo ya mchezaji bora chipukizi mwaka 2011 ambae kwa sasa anakipiga Los Angeles Clippers leo ni kumbukumbu yake ya siku ya kuzaliwa. alizaliwa tarehe kama ya leo na mwezi kama huu mwaka 1989.

Griffin alichaguliwa kuingia NBA kama mchezaji namba 1 kutoka Chuo mwaka 2009.

anakumbukwa kwa balaa lake alilolifanya pale alipoliruka gari aina ya KIA na kupiga Dunk la khatari


Kwa kuongezea Gang Chomba, mchezaji aliyemfuatia Griffin kwenye NBA draft ya mwaka 2009 hakuwa mwingine bali Hashim Thabit.
 
Back
Top Bottom