March 20, mwaka 1984 huko katika viunga vya
Fuenlabrada nchini Spain alizaliwa mshambuliaji ambae baadae alikuja fahamika kama El Niño.
Fernando Torres jina alilopewa na wazazi wake, alikuja kuwa mchezaji wa pekee kushinda mataji ya Champions League, Europa League, World Cup na European League championships.
alianza kutamba na Atretico Madrid, na badae akajiunga na Liverpool tokea mwaka 2007 hadi 2011 alipohamia Chelsea.
katika kukamilisha kipaji chake kama ambayo nyota wengine hufanya, Torres alihamia klabu yenye mafanikio zaidi Ulimwenuni yaani AC amilan.
Torres alitanabaisha kuwa kwa yeye kujiunga na Milan ilikuwa ni kukamilisha utukufu wake kwa wapenzi wa soka.
Historia yake inasema kuwa Torres alipokuwa mdogo aliimudu nafasi ya golikipa, na alijiunga na timu ya watoto ya Atretico mwaka 1995, kabla ya kuruhusiwa kujiunga na kikosi cha kwanza mwaka 2001 hapa sasa akiwa kama mshambuliaji.
aliifungia Atretico magoli 75 katika mechi 174 za La Liga.
akiwa bwana mdogo tu pale Atretico alifanikiwa kukivaa kitambaa cha unahodha na na kuwaongoza wachezaji wenzie waliokuwa wamemzidi umri na miongoni mwao alikuwa Diego Sumeone ambae kwa sasa anamfundisha hapohapo Atretico.
alipokuwa Liverpool alifanikiwa kuwa mchezaji wa kwanza kufunga magoli zaidi ya 20 kwa msimu tangu mwaka 1996. pia akawa mchezaji wa kwanza kufikisha magoli 50 kwa kipindi kifupi katika historia ya Liverpool.