Siku mbu akitua kwenye korodani zako ndiyo utajua kuna njia bora ya kutatua shida au matatizo bila kutumia vurugu

Siku mbu akitua kwenye korodani zako ndiyo utajua kuna njia bora ya kutatua shida au matatizo bila kutumia vurugu

Mhaya

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2023
Posts
1,831
Reaction score
5,489
Mungu alianza uumbaji wake katika siku ya kwanza.

Akaamua kuweka ardhi, lakini hii ardhi akaamua kuitofautisha, kwa nini? Kwa sababu alitaka dunia ipendeze. Akaiwekea miti na kwingine akaamua kupawekea mchanga mwingi na kupaita jangwa.

Kwingine akaamua kupawekea tu mchanga wa kawaida, ndipo tunapotumia kutembelea. Na kwingine akaamua kuweka maji mengiii, tunaita bahari, maziwa ama mito.

Mungu akaona haitoshi, akamuumba Adamu, aliiangalia dunia akaona haitopendeza ikiwa na mtu mmoja, tena wa aina moja, akamuumba Hawa. Yaani alitaka dunia iwe na watu wawili tofauti, waipendezeshe kama ilivyo sasa.

Mungu akaona haitoshi, watu wengine akawaumba wanene, wengine wakawa wembamba, wengine akawapa weupe, wengine akawapa weusi.

Wengine akawapa urefu, na wengine akawapa ufupi. Hapa kote Mungu anajaribu kuipendezesha dunia, iwe na vitu vya tofauti, na kweli leo tukiiangalia dunia, inapendeza.

Vipi Mungu angeiweka dunia nzima jangwa? Ama bahari? Dunia ingeonekanaje? Vipi Mungu angeumba watu wanaolingana vimo halafu wote wanene na wafupi? Dunia ingependeza? Vipi Mungu angeamua kuwaumba wanaume peke yao ama wanawake peke yao? Unaonaje hapo?

So ni lazima ujue ili mahali pachangamke, ni lazima kuwe na utofauti. Ukiingia mitandaoni na kukutana na habari za Simba tu, tena kusifiwa, yaani posti za Watanzania wote ni kuhusu Simba na kumsifia, hakika haipendezi, ili kupendeze ni lazima tukutane na posti za watu wanaoiponda Simba.

Hivyo hivyo hata kwa Yanga, kwa nini Tanzania nzima tumzungumzie Yanga kwa sifa kemukemu? Hapana, haitakiwi kuwa hivyo, ni lazima mitandao ipendeze kwa kuonekana watu wa kumkosoa.

Mimi nimefollow wasemaji wote wa Simba na Yanga. Sitaki kila muda nione posti za Ahmed Ally, wakati mwingine natakiwa nione posti za Ali Kamwe, nijue anasemaje.

Sitaki Instagram yangu ikae kibwege. Nimefollow wachungaji, nikafollow wanawake wavaa nusu uchi, nikafollow pages za sayansi, nikafollow page za dini. Nimefollow pages za mipira, nimefollow pages za muvi.

Nikiingia Instagram, nakutana na posti mbalimbali, tena tofautitofauti, inapendeza, ila ningekuwa nimefollow mpira peke yake, hakika ingeniboa sana.

Sasa watu wa Yanga tulieni. Oga, nenda kwenye mishemishe zako halafu jipangeni tena kama sisi tunavyofanya kila msimu. Kule Robo fainali watu hawacheki na kima, wanakuua tu kupitia VAR kama sisi tulivyofanywa katika ardhi ileile ambayo jana umeililia. Ni kawaida kwenye mpira.

Halafu mnashindwa kujua, hii mipira, ili ivutie lazima kuwe na udhulumishi kama huu, mechi iishe, umlalamikie refarii weee mpaka kesho yake. Labda baadhi yenu mmeanza kufuatilia mpira 2010.

Sisi tulioanza kufuatilia mipra tangu miaka ya tisini, tushazoea, na tuliamini hata VAR ikija bado kutakuwa na maamuzi ya kibinafsi. Tunayaona maamuzi haya mpaka Uingereza, tunalalamika weeee, mwisho wa siku tunatulia.

Bro! Huu udhulumishi ndiyo unalifanya soka lipendeze sasa.

Sema madogo wapo wengi sana siku hizi, wanapaniki kisa mpira. Watu wazima watakuwa wameelewa nini maana ya soka. Utafanyiwa fitina wee mpaka ukome.

Muulize Arsenal, kamuulize Liverpool, kamuulize Man United, kamuulize Chelsea, wote hawa wamepitia maumivu ya VAR halafu tunaona kawaida tu. Ila kutokea kwa Yanga, watoto walioanza kuangalia mpira mwaka 2015 wanalalamikaaaaaaaa.

DOGO! Jifunzeni soka kwanza. GROW UP!
 
Kichwa Korodani na Mbu
Mada Yanga na Malalamiko.

Huu mchanganyiko balaa. Ukiachiwa hata mgonjwa aliyepo koma ananyanyuka.
 
Jifunze kufupisha
mambo ni mengi na muda ni mdogo
Nitasoma kesho hii post yako
 
Back
Top Bottom