Habari wanajukwaa.
Kwanza kabisa namshukuru mwenyezi mungu kwa kunijalia Afya na kunipa wakati huu wakutoa mawazo yangu ambayo Huenda yakaleta athari chanya kwenye uchumi wa Tanzania yetu, Moja kwa moja nieende kwenye mada.
Kuna sehemu nyingi nimepita mikoani kuna majengo mengi yametelekezwa, Mfano majengo ya wachina wakati wanafanya ujenzi wa barabara za lami mengi yametelekezwa( Mfano wa hayo majengo yapo kigoma), Majengo ya Jeshi yametelekezwa( Mfano wa hayo majengo yapo Tabora, Brigedi ya FARU) Nini kifanyike Kuhusu Hayo Majengo HASA WAKATI HUU WA UHABA WA AJIRA???
Mosi, Kuna wahitimu wengi wa vyuo vya Ualimu kwanini wasipewe mkakati wa kuyatumia Majengo hayo kama madarasa.
Pili, Majengo hayo yanaweza tumika kama vituo vya Afya hivyo vijana wahitimu wa kada hiyo wakipewa majengo na mikakati ya kuanzisha vituo vya Afya inakuwa imepunguza uhaba wa Ajira kwa Asilimia Angalau 10% kulingana na utafiti wangu mdogo kwani kalibia kila mkoa yapo majengo hayo.
Tatu, Majengo hayo yanaweza kutumika na vijana MaIT waliohitimu pale UDOM au UDSM wakatengeneza maduka ya mitandaoni, Ukufunzi, Ufundi, na kuuza ujuzi wao juu ya mambo ya mitandao.
Nne, Sehemu hizo wapewe vijana kimkakati waanzishe, Maktaba za jamii na vyanzo vya Taarifa( Data resources Center) Watu wangapi watanufaika hapa?
Tano, Vijana waliohitimu ufundi wapewe maeneo hayo ili waanzishe ufundi wao ili wauze thamani na ujuzi wao ndani na nje ya nchi kuna mwaka nilikuwa naangalia Televisheni nikaona Nchi kama za Azbaijan wanaishi kwa kutegemea ufundi tu Fikilia tanzania tuna rasilimali ngapi ambazo zinatuwezesha kulipiku soko, Kumbuka baadhi ya miti wanayotengenezea huko ulaya, huitoa Tanzania.
Mwisho ni lai yangu kwa serikali na vijana hasa wahitimu tufikilie namna ya kupunguza uhaba wa Ajira, kwa utafiti wangu tu kama vijana watapewa Majengo yaliyotelekezwa wakaanzisha vitu vinavyoendana na ujuzi wao tatizo la Ajira litapungua kwa Asilimia 10% .
... itaendelea nikijadili ni mikakati ipi Serikali na vijana waje nayo ili kufaidika na majengo hayo.
ASANTE KWA KUSOMA ANDIKO HILI👏