Siku moja na Sheikh Ponda Mahakamani Morogoro 2015

Mazindu...
Kuna kisa ambacho hukijui.

EAMWS ilikuwa inajenga chuo kikuu mwaka wa 1968.

Bahati mbaya sana ikatokea fitna.

Pakawa na hofu kwa nini Waislam wawe na Chuo Kikuu?

Ukazushwa mgogoro mkubwa ndani ya EAMWS na serikali ilihusika katika fitna hii kwa kiasi kikubwa.

Serikali ikaipiga marufuku EAMWS na ikawaundia Waislam BAKWATA.

Mradi wa Chuo Kikuu na miradi ya ujenzi wa shule yote ikafa.

Kiwanja hiki kikawa sasa BAKWATA wanawauzia matajiri.

Pale Sheikh Ponda alipofikia kuchukua kiwanja katika hilo eneo ili ujengwe msikiti kiwanja chote kilikuwa kimemalizika kuuzwa.

Ponda alichukua sehemu ile ndogo ili angalau pawe kumbukumbu kwa ajili ya Sheikh Hassan bin Ameir.

Rudia kusoma kisa hiki utaelewa vizuri.
 
Last...
Mzee Waikela yu hai.
 
Sawa mzee wangu, nimekuelewa. Tuendelee na mjadara
 
Last...
Mzee Waikela yu hai.
Afadhali.. udongo wa mjerumani ule. Nadhani atakuwa na miaka 90 na zaidi sasa. Alikuwa rafiki mkubwa wa Babu yangu. Akinituma nimpelekee barua ya vikao mbalimbali Tabora miaka ya 90 mwanzoni. Namjua vizuri. Mwamba sana yule mzee
 
Afadhali.. udongo wa mjerumani ule. Nadhani atakuwa na miaka 90 na zaidi sasa. Alikuwa rafiki mkubwa wa Babu yangu. Akinituma nimpelekee barua ya vikao mbalimbali Tabora miaka ya 90 mwanzoni. Namjua vizuri. Mwamba sana yule mzee
Last Emperor,
Kuna watu wanne katika historia ya Tanganyika ambao wamekabiliana na Julius Nyerere uso kwa macho baada ya kupishana katika mambo muhimu ya siasa katika TANU na wakasema maneno makali.

Mtu wa kwanza ni Sheikh Suleiman Takadir (1958), Titi Mohamed (1963),Bilali Rehani Waikela (1963) na Schneider Abdillah Plantan (1965?).

Hakika Bilali Rehani Waikela ni mwamba.

Yeye alikuwa katika kamati ya Waislam iliyochaguliwa kufanya sulhu kati ya EAMWS na kundi dogo la Waislam wenye nguvu na ushawishi mkubwa ndani yaTANU na serikali ambao walikuwa wanataka EAMWS ivunjwe.

Kiongozi wa kamati hii alikuwa Mussa Kwikima.
Baada ya kushindakana kupatikana sulhu serikali iliivunja EAMWS na kuunda BAKWATA.

Baada ya hapo ikatoka amri kuwa nyaraka zote za mgogoro ule zichomwe moto zisiwepo na atakaekutwa na nyaraka hizo atashughulikiwa.

Inaelekea wajumbe wa kamati ile wote walizichoma moto nyaraka zao.
Bilal Rehani Waikela yeye nyaraka zake alizificha mahali kwa muda wa takriban miaka 20.

Katika miaka ya 80 alizichukua nyaraka zile akampa kijana mmoja kutoka Tabora jina lake Mohamed Lulengelule ambae alikuwa mwanafunzi wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam na kiongozi wa Muslim Students Association of the University of Dar es Salaam (MSAUD) azifikishe Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam zihifadhiwe.

Hivi ndivyo mimi Nyaraka za Waikela zilivyoweza kunifikia na nikazisoma zote.

Nyaraka hizi ni ''minutes'' za mikutano, taarifa za kamati, ''cuttings'' za magazeti The Nationalist, Tanganyika Standard nk. nk.

Kutokana na Nyaraka za Waikela nikaandika paper, ''Islam and Politics in Tanzania,'' (1989) paper ambayo niliwasilisha kwenye mkutano Nairobi mwaka wa wa 1989.

Unaweza kuipata hapa: “Islam and Politics in Tanzania,” (1989) Al Haq International Karachi, Vol 1/No. 3 August - December, 1993.

Hii paper nimeitia kama sehemu ya tatu na ya mwisho katika kitabu cha Abdul Sykes.

Nilikutana na Mzee Waikela nyumbani kwake Gongoni Tabora na elimu aliyonipa kuhusu uhuru wa Tanganyika na mchango wa Waislam nisingeweza kuipata popote.

Hakika nakubaliana na wewe unaposema Mzee Waikela ni mwamba.
Mimi nakuongezea lingine Mzee Waikela ana hazina kubwa kichwani kwake.

Laiti kama asingehifadhi zile nyaraka historia ya kuundwa kwa BAKWATA isingefahamika.
 
HAKIKA!!!
 
Kwa uelewa wangu hizo mali za Waisilamu kwa kipindi hicho hazikutakiwa kupelekwa BAKWATA kwa kuwa BAKWATA sio Serikali. Ilitakiwa zibinafsishwe na zirudishwe Serikalini kama ilivyofanyika kwa mali zilizokuwa zinamilikiwa na Madhehebu ya Kikristo.
 
Kwa uelewa wangu hizo mali za Waisilamu kwa kipindi hicho hazikutakiwa kupelekwa BAKWATA kwa kuwa BAKWATA sio Serikali. Ilitakiwa zibinafsishwe na zirudishwe Serikalini kama ilivyofanyika kwa mali zilizokuwa zinamilikiwa na Madhehebu ya Kikristo.
Mawe...
Ilikuwapo sheria kuwa mali zinauzwa na kinachopatika kinagawiwa wanachama.

Serikali haikuweza kufanya hili hivyo ikatungwa sheria kuwa mali za EAMWS zikabidhiwe BAKWATA.
 
Pole sana Mzee naona ukiwa jirani kabisa na Mzee Waikela
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…