Siku nikipata kazi nitaruka kama ndama.

Siku nikipata kazi nitaruka kama ndama.

kante mp2025

JF-Expert Member
Joined
Nov 11, 2022
Posts
631
Reaction score
1,192
Mimi ni mgonga ulimbo mwenye matumaini tele wakati wagonga ulimbo wenzangu wakiwa addicted na porn na betting.

Basi mimi niko addicted na page & website za sekretarieti ya ajira maana nina imani nao sana tu baada ya mgonga ulimbo mwenzangu kutoka kule Inyalikungu kulamba shavu kwenye moja ya taasisi nono tu bila connection yeyote zaidi ya Mungu wa mbinguni sasa hivi anajilia marupu rupu kama mpumbavu pale maabara kuu ya taifa NIMR.

Nikiwa kama mmoja ya wagonga ulimbo baada ya kuona website inasoma 0 job vacancy kiukweli nikama nimepigwa msumali wa kichwa naamini mambo yatanoga tena ili niendelee kurusha nyavu labda zitanasa.

Wakuu wa sekretarieti ya ajira washawahi nibutua risasi ya kichwa kwenye written interview moja nikalamba 38 kama mpumbavu nililia kama kichanga sikuwakatia tamaa nikarudi tena kupambania moja ya nafasi zao nikafanikiwa kufika oral

Sasa lile neno la selected for oral linalipa matumaini sana ila kimbembe ni kuwa kila nikifungua pdf za placement najikuta sipo, Hapa namwomba Bwana Wa Majeshi na Mizimu ya Makumbusho Inifanyie Muujiza nami niwe miongoni mwa hawa wanaopata placement.

Natanguliza Shukrani, Kutokea Mpimbwe DC
Screenshot_20250124-190050.png
 
Ok. Komaa mkui ila umri haukungoji na mtaani vibarua vya kubeba taka vinalipa sana tena hasa ushuwani
 
Back
Top Bottom