POTIZILLAH
Member
- Apr 30, 2011
- 87
- 158
Siku moja nilikua nimeenda kumtembelea mshikaji wangu mmoja Mwenge, yeye ana duka lake la nguo mitaa ile. Sasa story story hadi mida ya mchana tukaona twende tukapate lunch.
Katika mgahawa mmoja mitaa ya jirani na ofisi ya mwana. Palikuwa pamejaa sana, meza tuliyokuta tupu ilikua na mtu mmoja (kila meza ilikuwa inachukua watu wanne) basi tukakaa hiyo meza yenye huyo jamaa ambae yuko peke yake na ikabaki siti moja. Tukiwa tunaendelea na misosi yetu akaingia dada mmoja, baadae ndio tulikuja kujua kuwa yule mwamba wa meza yetu alikua anamsubiri huyo binti ni mwanamke wake, ila kuna kitu mimi sikua najua kabla kumbe jamaa yangu nae yule dada ulikua ndio mchepuko wake rasmi, yaani ni kama bi mdogo wake (jamaa ameoa na ana watoto wawili)
Sasa tokea akiwa kwa mbali (mlangoni mpaka meza zilipo unatembea kama hatua kumi hivi) jamaa wa meza ya nyuma akawa anapiga story kuhusu huyu dada kwa sauti ambayo hata sisi wa meza yetu wote tulikua tunasikia, "UNAMUONA HUYO DADA ANAEKUJA, ALIKUA ANALIA SANA PALE HOSPITAL. NI MJAMZITO SASA WALIVYOKUA WANAMPIMA KUJUA HALI YAKE YA AFYA WAKAGUNDUA KUWA PIA ANA HIV, DADA ALICHANGANYIKIWA SANA AKAWA ANALIA KAMA KAAMBIWA ANAKUFA LEO. MANESI WAKAMTULIZA WAKAMWAMBIA AMUITE MUME WAKE ILI WAJE WAPIME WOTE. DADA AKAMPIGIA JAMAA AKAJA PALE AKAMPOZA POZA DADA WAKAINGIA VYUMBANI TENA (Jamaa alieitwa hata hakua mmoja kati ya hawa wana niliokua nimekaa nao mezani) NAONA WAKATOKA DADA AMETULIA
Sisi kwanza kukamgeukia anaeongea, kisha kwa pamoja tukawa tunamuangalia dada. Dada kumbe alivyotulia alimpigia simu huyu jamaa mwingine tuliekaa nae, wakaongea kuwa watakutana hapo kwenye mgahawa, ila dada alivyoona mabwana wake wawili wamekaa meza moja akajua hapa nitaharibu akawa anamuitia yule jamaa yake nje. Yule jamaa kumbe kisha panic, akaanza kumrushia matusi hapo hapo.. UMENIAMBUKIZA UKIMWI na maneno kibao, watu wakamtuliza wakawatoa nje. Waliachana pale pale kila mtu na njia yake. Nikaona jamaa yangu ananiambia twende zetu nikajua ni kwakuwa ameona pale pana maugomvi basi ndo anataka tuondoke.
Nikaona hatuelekei dukani tunaenda njia ya TRA palikua na bar moja ilikua inaitwa BM, akaniambia tukae pale, basi tukawa tunakula vitu ila naona jamaa ana mawazo sana ila anapiga story nyingine anajichekesha ila usoni unaona kabisa huyu mwamba hayupo sawa. Bia hazipendi uongo basi bia ya nne tu jamaa akaanza kunipa story ya yule binti. Eti alikua ni mwanamke wake wa muda mrefu sana na hata ile mimba ana habari nayo na alijua ni yake. Sasa kuwa ina baba watatu na kuwa dada ni HIV positive vilimchanganya sana mwana. Basi nikampoza poza tukapiga story nyingi sana kuhusu lile suala
Ila kilichonifanya nijisikie vibaya kuliko vyote hata hakua huyu jamaa yangu, ila ni yule mwamba wa pale hotel ambaye alisababisha ugomvi pale hotel, jinsi alivyokua anaipokea ile story kutoka kwa huyu msimuliaji na vile anamuona yule dada pale, nahisi angekua na chance angemuumiza sana yule dada. Ila hata huwezi jua labda yeye ndio chanzo cha tatizo, labda yeye ndio kaambukiza wote labda kama walipima yeye na dada kabla hawajaamua kuanza kulana kavu na akawa ameachana na mambo mengine yote ya pembeni na ametulia na dada tu. Ila dada kwangu ndio nilimuona ni tatizo maana hapa tu tunaowajua ni watatu bado tusiowajua
MORAL SIDE OF THE STORY: Tutulie na wapenzi wetu na kama hatuwezi tutumie ndom