JEJUTz
Member
- Aug 22, 2024
- 75
- 197
Hii siku haitokaa niisahau abadan!
Ilikuwa ni baada ya kushiba chakula changu cha mchana hapo home,huku nikifanya michezo ya hapa na pale.
Ghafla nikakutana na kiberiti cha gesi nikakifuata na kukichukua. Ile zima washa zima washa ikanivutia nikaamua kwenda nacho mtaani.
Kulikuwa na open space yenye nyasi ndefu kwenye eneo kubwa tu karibu na makazi ya watu, huku zikiwa zimekauka vizuri kwa jua kali.
Basi bhana nikajongea hapo na kiberiti changu cha gsi. Nikawa nawasha moto kisha nazima.Mara ghafla moto ukanizidi nguvu .
Nikaona isiwe taabu nikatimua mbio mpaka mtaa wa tatu huko.
Moto ukawa mkubwa vibaya mno, huku ukitishia usalama wa raia, mali pamoja makazi yao.
Hakika watu walipambana na kushughulika vya kutosha. Huku wasijue nani kasababisha janga lile. Bahati nzuri moto ulidhibitiwa na kuleta madhara kidogo tu.
Je! wewe ulifanya tukio gani ukiwa mtoto ambalo hutolisahau?