Siku niliyokutana na jini kwenye daladala

Kuna anko wangu alinisimulia kuwa alienda kumfata jamaa nyumbani kwake akafunguliwa mlango na mwanamke (mke wa huyo jamaa) akamjibu kuwa mwenyewe amelala , alivyoondoka mbele anakutana na jamaa huyo huyo anatoka kwenye mizunguko yake ,akamuuliza kuwa nimekuja kwako nimeambiwa umelala ,jamaa akashangaa akamwambia mi mbona muda sipo nyumbani na mke wangu amesafiri ,mlango nineondoka nimeufunga....jamaa akashindwa kuelewa huenda alikuwa ni jini ama laa.

Pia kuna ndugu mmoja alinunua kiwanja akajenga nyumba , ila ile nyumba ilikuwa haikaliki .alimuweka ndugu yakee mmoja akae ila anasema alikuwa akikaa anaona kuna mwanamke anapita humo ndani usiku na mchana. Ila akienda kumtazama hamuoni. Baadae akaja kufatilia akaambiwa kuwa hilo eneo kabla hajalinunua alikuwa akiishi huyo jini so anagoma kutoka cuz pale anapaona ni sehemu yake.
 
SEHEMU YA 09
****************************************
Ilipoishia ni pale fetty amekuja nyumbani pale amekuja na gari aina ya v8 amesema gari ilo nimepewa liwe langu na babaake na ameniambia wazazi wake wamefurahia mimi kwenda kuwaona kule ujinini japo nilikuwa naona kama naota kumbe nilienda kweli ujinini kule,
Na pia fetty akaniambia kuwa sasa tupo kwenye vita kubwa mno na adui yetu ni salome?
Maneno yake yalinishangaza kajuaje kama niliwasiliana na salome yule classmates wangu ambae alikuwa nasoma nae secondary kizuka morogoro,
Nikamuuliza kuna vita gani ?
Akasema ww utaona tu sema hawezi kunishinda
Nilishangazwa sana na maneno yake sasa akawa ananiambia ili gari ni lako kuanzia sasa na zimebakia siku 3 mimi na wewe kuanza kuishi pamoja lakini pia nampango wa wewe kuhama hapa twende tukaishi masaki,
Nikamuuliza tukaishi masaki kule nitawezaje kulipa kodi wakati kule ni eneo wanaloishi matajiri ?
Akacheka sana akaniambia usijali kwa kuwa mimi nipo hakuna chochote kisichowezekana basi nikasema sawa basi siku hiyo alilalaa kwangu tulifanya mapenzi kama kawaida sasa asubuhi yake aliniambia anaondoka anaenda kwao ujinini ilq baada ya siku moja atarudi nikamwambia sawa,
Basi kweli mida ya saa tano tano asubuhi aliniaga kuwa anaondoka ila alinitaarifu niache kabisa kuwasiliana na salome nikamwambia sawa akaendelea kusema kama utakaidi maagizo yangu kitachokukuta usije ukanilaumu baadae.
Nikamwambia sawa kweli alitoweka mbeleni mwa macho yangu alipotea ghafla simuoni akawq ameondoka hivyo basi nilibakia na mawazo sana sijui hatma ya maisha yangu nikajisemea kimoyo safari hii nimepatikana,
Sasa nikatoka nje kwenda kucheki lile gari aliloniletea fetty kwasababu alinikabidhi kila kitu hadi funguo nilifungua mlango nikaingia ndani wapangaji wezangu wote walikuwa wananishangaa sana kuona nimeletewa gari ni gari zuri sana nilikuwa siwezi kuendesha vizuri niliwasha tu pale nikawa napiga piga hodi tu furaha niliyokuwa nayo sio ya kitoto nilikuwq najisemea na mimi leo namiliki gari upepo uliokuwepo mule ndani ya gari ulikuwa ni ka upepo mwanana nilijikuta nahasau mateso yote ya yule jini nikawa naona raha sasa nikiwa nipo mule ndani ya gari nikaangalia siti ya nyuma nikaona begi jeusi nikasema ngoja nilifungue lile begi sikuamini nilipokutana na kibunda cha hela na kulikuwa na simu kubwa smartphone moja nzuri ikabidi nilitoe ilo begi niingie nalo ndani sasa nilipoongia ndani nikazihesabu zile pesa zilikuwa shs millioni moja nikaiwasha ile simu ilikuwa ni smartphone kampuni ya samsung sikuwa mzoefu na masuala ya smartphone niliiwasha tu ikawaka sasa cha ajabu pale kwenye wallpaper ya simu nikaona kuna picha imeseviwa pale nimepiga picha na yeye fetty tumekumbatiana na sijui ni mahali gani hapo hiyo picha sikumbuki tulipiga wapi nikashangaa sana sasa wakati nipo na mawazo nusu nikimbie nilipoona simu hiyo niliyoishika imeanza kuitaa namba imeseviwa mke wangu mpendwa nikawa sijui pa kupokelee ilipiga mara ya kwanza ikakata tena ghala simu yangu ndogo ikaita nikaona jina fetty nikapokea akaniambia mume wangu umeziona zawadi zako mule kwenye gari nikasema ndio akasema nakupenda sana hiyo simu nimekununua kuanzia sasa utakuwa unatumia hiyo simu kubwa najua haujui kuitimia kesho nitakapokuja nitakuja kukufundisha sawq nikasema sawa akasema na hiyo hela millioni moja ni mtaji wako wa biashara utakayotaka kufungua tafuta biashara ufungue nikasema sawa akasema kesho nitakapokuja nakuja kukuchukua tunahama hapo tunahamia masaki na hivyo utakapokuwa masaki inabidi utafute biashara ya kufanya ndio maana nimekupa hiyo millioni moja ishu ya kodi usiwaze mimi nipo akamalizia kwa kusema nakupenda sana ila najua tupo kwenye vita kubwa ila hawezi kushinda vita maneno yake yalikuwa yakinishingaza sana kwann fetty anasema tupo kwenye vita nikwambia mke wangu unanitisha sana unaponiambia tupo kwenye vita akacheka akasema haujui tu ww ni binadamu haujapewa uwezo wa kuona mambo ya mbele yanayotokea akasema usijal lakini kesho utaniona akakata simu,
Aliniacha na mshangao sana kwann anasema maneno yale basi wakati tu amekata simu ghafla simu yangu ikaiita nikajua ni yeye anapiga tena lakini safari hii mpigaji alikuwa ni salame,
Nikajisemea salome anataka nini tena ikabidi nipokee simu....

Wakuu nitaendelea muendelezo

Sent from my SM-J260T1 using JamiiForums mobile app


MUENDELEZO Soma Siku niliyokutana na jini kwenye daladala
 
Tunasubiri
 
Mwambie afuge nguruwe tu.
 
Waajemi ndiyo wajenzi namba moja duniani wakifuatiwa na Wahispania. Wahenga waliwasiliana na mizimu na majini katika kutoa maamuzi na kufundishwa miundo mbinu.
 
Kali sana hii mkuu

Sent from my TECNO K8 using JamiiForums mobile app
 
Kweli mkuu sema sio kama mimi mzushi ila muda nakosa mkuu wife kajifungua ndio shida yaani ninapopata mda kama hivi ndio naingia jf ila nitajitahidi angalau tuimalize stori
Kwanini waleta story wote huwa katikati ya story mnapata emergency?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…