Siku niliyokutana na jini kwenye daladala

Upumbavu tu hapa stori za uongo tu, mambo ya sjui kupendwa na jini sjui nini ni upuuzi na uongo mtakatifu , na watu wanakesha kubebembeleza mtu aendelee kuwadanganya na stori za abunuasi
Pumbavu kabisa.
[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Upumbavu tu hapa stori za uongo tu, mambo ya sjui kupendwa na jini sjui nini ni upuuzi na uongo mtakatifu , na watu wanakesha kubebembeleza mtu aendelee kuwadanganya na stori za abunuasi
Pumbavu kabisa.
Nlichogundua watu kama wewe mliwapata majini madume yakawageuza wake zao ndo mana mnamind na kuwa na hasira...,tulia zali lako lilikua baya mwana kapata zuri
 
Upumbavu tu hapa stori za uongo tu, mambo ya sjui kupendwa na jini sjui nini ni upuuzi na uongo mtakatifu , na watu wanakesha kubebembeleza mtu aendelee kuwadanganya na stori za abunuasi
Pumbavu kabisa.
Unafanya nini kwenye huu uzi sasa...au unataka kufanywa
 
Hapa Tangawiz imezidi kidogo kama V8 gar ndogo itakua huko ujinini wanatumia ma buldozer
Mkuu mimi Nina Lexus saloon inafanana na crown ni V8 na cc 4000. Just google Lexus LS 400 utaiona kwa mara ya kwanza maana najua hujawahi kuona na ni chache mno
 
SEHEMU YA 11
************************************
mwajabu yule rafiki wa jini fetty ambae yeye alikuwa ni binadamu tu kama sisi alinisimulia jinsi walivyokutana na fetty hadi hivi sasa wamedumu na urafiki wa miaka 10 pamoja ni ngumu kuamini kama jini na binadamu wanaweza kuwa na urafiki tena wa mda mrefu hivyo,
Mwajabu anasema alikutana na fetty katika mazingira magumu mno miaka 10 iliyopita ilikuwa hivi mwajabu anasema alikuwa akienda zanzibar kwa mamaake mdogo kila mwisho wa mwaka kumsalimia mamaake huyo mdogo sasa siku moja anasema uwa yeye ni mtu wa kupenda kwenda kwenda beach sasa siku moja ameenda zake beach na mtoto wa mamaaake mdogo wapo beach kule kule zanzibar sasa yeye alikuwa amejitenga kidogo alikuwa akizunguka zunguka pale beach ghafla wakati anazunguka akaona kuna chupa inaelea baharini sasa ikabidi aifuate ile chupa sasa ile chupa ilikuwa ni chupa ya soda ambayo ilikuwa na kizibo akaanza kuifungua anasema alipoifungua alishangaa kuona moshi umetoka mule ndani ya chupa kitu kilichomshtua na kuitupa ile chupa akakakimbia na kumwambia yule ntoto wa mamaake mdogo waondoke haraka anasema hapo ndipo rasmi jini fetty alipokutana nae anasema baada ya kupita kama wiki siku moja alikuwa anatoka sehemu usiku anarudi kwa mamaake mdogo ghafla akawa amevamiwa na vibaka wanne walitaka kumbaka katika purukushani za kupiga piga kelele ghafla akatokea mdada mmoja asiemfahamu yule mdada alipotokea akawaambia wale vibaka naombeni mumuache huyu binti haraka anasema alishangaa wale jamaa wakimuacha na kukimbia kitu kilichomshangaza sana anasema baadae yule dada alikuja karibu yake huyo ndio fetty akamwambia usijali nimekusaidia kwa kuwa uliwahi kunisaidia sasa nenda nyumbani anasema alishangaa sana akaondoka kurudi nyumbani zikapita siku na masiku akawa amerudi tz sasa yeye kwao ni dar mbagala rangi tatu anasema akiwa dar alikuwa akitafuta kazi za ndani sana siku moja akapigiwa simu na namba ngeni anasema huyo aliempigia simu alimwambia nasikia unatafuta kazi za ndani kazi umepata kwangu kesho tuonane basi ikabidi siku hiyo wakutane anasema alishangaa anakutana na yule yule dada aliewahi kumsaidia asibakwe kule zanzibar kwa kuwa sura yake aliikumbuka hapo ndipo alipopata kazi za ndani kwa fetty rasmi
([emoji849][emoji849][emoji849][emoji849][emoji849][emoji849][emoji849][emoji849][emoji849][emoji849][emoji849][emoji849]MSHANGAOOOOO)
####
STORI ni ndefu sana juu ya mwajabu kukutana na jini fetty huyo yote mwajabu alikuwa akinisimulia kipindi kile anasema fetty aliwahi kupewa adhabu ya kuwekwa kwenye chupa na ile siku ameokota ile chupa ndio alipomfungulia fetty bila kujua anasema fetty alimwambia kuwa yeye ni jini na siku ile amemfungulia mule kwenye chupa alikuwa yupo katika adhabu kali ambapo anasema hiyo adhabu alipewa na familia moja ghafla mwajabu alisita kuendelea na simulizi akaniambia tuachane na hii stori ikabudi nimuulize kwann akasema naona fetty hapendi mimi kukwambia ukweli na kama nikiendelea atanipa adhabu na mimi na fetty tumekaa miaka mingi bila ugomvi na amekuwa akisomesha ndugu zangu akiisaidia familia yangu akawa anaongea kwa kulia kuwa fetty amemjengea nyumba pale tabata anapangisha ni mengi mazuri fetty amenisaidia kwa kulipa fadhila ndio maana ameamua tu kuishi nae humu humu ndani baadae mwajabu akasema shem kama unampenda fetty ww ishi nae kwani ni mtu mzuri sana japo uwa ana hasira za haraka na kali mno,
Mwajabu alimaliza simulizi yake hivyo japo hakuniambia ni familia ipi iliyompa adhabu kali ya kumuweka kwenye chupa jini fetty,
#SASA ENDELEA#
Maisha yangu na fetty mule ndani yaliendelea vizuri nikawa na maisha mazuri sana tulikuwa tukipenda na fetty kule ujinini kwao hadi nikawa nimezoeleka na ndugu zake wote na niliweza kufungua biashara kariakoo ya kuuza vifaa vya umeme nilikwa na maisha mazuri kiasi cha kununua uwanja na kujengea wazazi wangu nyumba ndogo ya vyumba vitatu ya bati nzuri maisha yakasonga sasa tuliweza kuishi miaka 2 kwa amani na fetty sasa nakumbuka siku moja sitaisahau ni pale nilipoiona namba ngeni ikinipigia simu nilikuwa nipo kazini ikabidi nipokee simu sikuamini kama ni salome na bado ananifuatilia licha ya kumblock namba zake ni kajisemea huyu binti hachoki tu kunitafuta nakumbuka salome siku hiyo aliniambia kuwa nimeoteshwa unazidi kuingia pabaya na maisha yako sasa yapo katika hatari mno achana na fetty nikamjibu kuwa kuachana na fetty siwezi na yeye afuate mambo yake na huyo mungu wake kama amekosa kazi aje nimpe ajira
Licha ya maneno haya salome hakukoma kunitafuta,

Wakuu nitaendelaa


MUENDELEZO Soma Siku niliyokutana na jini kwenye daladala
 
Safi, ila mkuu fanya iwe hata ndefu kiasi.
 
Mkuu mimi Nina Lexus saloon inafanana na crown ni V8 na cc 4000. Just google Lexus LS 400 utaiona kwa mara ya kwanza maana najua hujawahi kuona na ni chache mno
Hongera kwa kupambana kulinywesha mafuta Hilo dude la CC4000. Sio mchezo mkuu kama unalimudu basi wewe ni uchumi wa Kati grade 1.
 
Hongera kwa kupambana kulinywesha mafuta Hilo dude la CC4000. Sio mchezo mkuu kama unalimudu basi wewe ni uchumi wa Kati grade 1.
Nililimudu kabla sijatumbuliwa..badaae nikabadili engine nikaweka Beams 2000
 
Kumbe hizi habari za jini kwenye chupa hazikitutungwaga tu... Aisee kweli maisha yanamengi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…