Siku niliyokutana na jini kwenye daladala

Siku niliyokutana na jini kwenye daladala

He! Sijaingia wiki nikijua ntakuta episode 5 hivi kumbe uzi umetelekezwa
Yuko zake ukweniiii kwa kina fetty......mwanzo alisema anahudumia my wife wake kajifungua labda ndo maana....fetty nae si alikuwa na mimba sa ilikuwaje hajasimlia ile mimba adi akafikia kutafuna mwajabu🤣🤣🤣🤣🤣
 
Majini walikuwepo enzi na enzi... wanajua mengi na ndio maana wapo kwenye dini ya haki..... Wao wana ufaham na uelewa mkubwa wa mambo.
Hao jamaa ni wafuasi wa shetani, sasa kama wako kwenu jaribu kujitafakari vizuri. Kumbuka mnasema kuna majini wazuri na wabaya, ukifa utapewa mabikira 72 [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23], hizi dini bhana
 
Au nae wamempa adhabu ya kufungiwa kwenye chupa...ngoja niende coco beach
Wakuu habari za humu jf ndugu zangu? Nilipata msiba ndio maana sikuwepo jf mtu aliefariki ni mtu wangu muhimu katika maisha yangu ila nimeshapoa kesho nitaendeleza stori asubuhi kama kawaida [emoji122][emoji122]

Sent from my SM-J260T1 using JamiiForums mobile app
 
SEHEMU YA 13
********************************
Wakati nipo kitandani pale kwenye kitanda ninacholala na mke wangu jini fetty safari hii nilikuwa nipo na mwanamke mwingine tena rafiki ake fetty, mwajabu tukifanya yetu ghafla nilisikia sauti ikiniambia haya ndio malipo uliyoona kunilipa kwa kutembea na rafiki angu?

Ilikuwa ni sauti kubwa iliyoongea kwa kujirudia rudia kiasi cha kunifanya niianze kuogopa nilikuwa nikitetemeka sana lakini cha ajabu mwajabu yeye alikuwa hasikii hiyo sauti kitu kilichonishangaza,

Ile sauti ikasema chochote kitachotokea kwako usije nilaumu kuanzia sasa ghafla sauti ile ikawa imekata kabisa,
Nilimwambia mwajabu aondoke arudi chumbani kwake mwajabu aliniuliza kwann kinqongea kwa sauti ya ukali naomba uondoke humu chumbani kitu kilichomshangaza mwajabu ikabidi aondoke mara moja,

Basi nilijikuta tu nalia macho mengi mule chumbani kwa kitendo cha kumsaliti fetty nilijua sasa huenda nitakuja kupewa adhabu kali ile sauti iliyokuwa ikiongea ilinithibitishia kuwa ile ilikuwa sauti ya fetty nililia machozi kuomba msamahaa kwa kufanya kosa lile nikajaribu kuipiga simu ya fetty laikini ilikuwa haipatikani tuma meseji hazijibiwi nikabaki sina la kufanya,
Usiku wa siku hiyo ulipita kama upepo ,

Asubuhi nimeamka sikuwa hata na mood ya kwenda kazini pale dukani kwangu kariakoo siku hiyo niliamka mwili wote unaniuma sana niliona kama mgongo wangu haufanyi kazi kitu kilichonishangaza sana nikatamani kuamka lakini nilishindwa nilipiga kelele kumuita mwajabu aje lakini kelele zangu zilikuwa kama kumpigia mbuzi gitaa nikawa najiuliza mgongo nimefanyaje hau nimepalalaizi? Nilishindwa kuamka kitandani ikabidi nijidondoshe chini ili nianze kutambaa kwenda kwenye chumba cha mwajabu mgongo ulikuwa unaniuma sana nilikuwa nikijikokota kota kota kidogo hadi nikafanikiwa kwenda chumbani kwa mwajabu ndugu msomaji nilikuwa nikitembea kama mlemavu kwa kutembelea mikono sasa nikakuta chumba cha mwajabu kipo wazi mlango umefunguliwa nikawa naita mwajabu mwajabu mwajabu lakini sikusikia sauti ikinijibu ikabidi nijikokote niingie ndani ile nimeshaukaribia mlango wa chumba mwajabu kupiga jicho ndani ya chumba cha mwajabu nilishtuka kuuona mwili wa mwajabu upo chini macho yalikuwa yametoka nje huku mdomoni nwake mapovu mengi yalikuwa yakimtoka nilishtushwa sana nilililia sana ikabidi nijikokote hadi mule ndani kweli mwajabu alikuwa kafariki nilipoufikia mwili wake vizuri niligundua pembezoni mwa shingo yake kulikuwa na alama za kukwaluzwa kwa kucha kali sana na nilipoangalia vzr niligundua mwajabu hakuwa na damu mwilini mwake nikagundua uenda nwajabu alikuwa ameuwawa kikatili nikajiuliza ni nini hiki?

Wakati nipo nashangaa haya yote ghafla mlangoni kikatokea kiumbe kama mtu lakinu alikuwa anqfanana na sokwe alikuwa na kucha nyingi mno pia alikuwa bonge la sokwe na alikuwa amejaa damu mdomoni nikapata hofu nikqanza kutetemeka lile jitu likaanza kunifuata mule chumbani nilitamani kukimbia lakini uwezo huo sikuwa nao nikawa napiga kelele lile jitu liliponikaribia likacheka sana kwa sauti kubwa tena iliyokuwa ikikwaruza kwaruza nikajisemea leo nakufa lile jitu ghafla likaanza kunywea taratibu likabadilika sekunde kadhaa nilimuona fetty kumbe fetty alijibadilisha na kuwa lisokwe lile fetty akaanza kucheka na kuniambia haya ndio malipo yako ww kijana mpumbavu akaendelea kusema huyo mpumbavu hapo chini mimi ndio niliemuua jana usiku bado zamu yako ww nitakuua taratibu taratibu nilikwambia usije nisaliti lakini haukusikia fetty alikuwa akiongea kwa uchungu mno nikaanza kumuomba msamahaa kwa kulia laini fetty alikuwa anisikilizi.


Itaendelea wakuu leo usiku
 
Back
Top Bottom