Siku niliyokutana na jini kwenye daladala

Siku niliyokutana na jini kwenye daladala

handsome boy wa jf

Senior Member
Joined
Jan 2, 2022
Posts
163
Reaction score
350
Moja ya kitu ambacho sitaweza kukisahau katika maisha yangu ni siku niliyokutana na jini kwenye daladala nakumbuka ilikuwa ni mwaka 2019 wakati nipo Chanika nilikiwa natoka kariakoo narudi ghetto ilikuwa ni mida ya saa 1 usiku sasa nikiwa kwenye gari akaja mdada mmoja akapanda kwenye dala dala niliyokuwa alikuwa ni mzuri amevaa kiostadhat sasa kutokana na ufinyu wa siti hakupata nafasi ya kukaa sasa sijui ni nini kilinipata uwa sina desturi ya kumuachia mtu siti hata awe mzee hau mgonjwa vipi maana mimi ndio utaratibu niliojiwekea naheshimu sana nauli yangu.

Sasa nikajikuta namuhurumia yule dada nikamwambia njoo ukae hapa mimi nashuka mda sio mrefu akatabasamu na kuja kukaa na kushukuru nikawa nimesimama safari ikaendelea ila niligundua yule dada alikuwa akinitazama kwa kuniibia ibia nikimtazama anajifanya ananipotezea basi safari ikiwa imekolea nikiwa nimekaribia chanika yule dada akaniambia kaka samahani nashukuru kwa moyo wako ulionionyeshea wa kunisaidia kukaa naweza pata nambaako ya simu kama hautojar?

Swali ili lilinishangaaza sana mwanaume yoyote lazima upagawe unapoombwa namba ya simu na mwanamke mrembo unakuwa kama haumini amini nilipatwa na furahaa nikampa akaniambia ahsante mimi naitwa fatmah ww unaitwa nani nikamjibu naitwa flani basi mazungumzo yakata kata hadi niliposhuka mimi sikumfuatilia tena nikaendelea na mishe zangu safari ya kwenda ghetto kwangu sasa nilipofika ghetto ikanibidi nioge halafu nipumzike maana nilikuwa nimechoka sana siku hiyo sasa nikiwa katika wimbi la usingizi mzito nikawa namuota yule dada niliekutana nae kwenye gari alikuwa amekuja kwangu yupo mlangoni anagonga huku akiiniita ww kaka mpolee hodii hoddiii aligonga sana ikabidi niamke niende kumfungulia nikamuona amevaa nguo nyekundu tukasalimiana hapo nipo ndotoni ndio naota hivyo akaingia ndani akaa kwenye sofa tukawa tunapiga stori nikamuuliza

Aisee siamini kwangu umepajuaje akasema aliulizia ulizia mtaani akaelewekezwa halafu isitoshe yeye anaishi karibu na mimi nikamuuliza ww unakaa wapi akasema mimi ni mgenu hapa mtaani nimekuja kwa dadaangu anaitwa sakina nikasema sakini yule mwenye saloon hapo mbele?

Akasema yeeah kumbe unamfahamu nikamwambia yule ni maarufu sana hapa mtaani akatabasamu akawa anafurahi tu chini chini sasa ndoto yangu ilikuja kuaribiwa na panya mmoja ambae aliangusha kitu ipo hivi kipindi nakaa chanika ghetto ghetto langu nilikuwa nasumbuliwa na panya niliwatega na dawa lakini wapi sasa nilishtushwa na kusikia sufulia limedondoka ikabidi niamke kumbe panya kuwasha tochi panya akakimbia ikabidi nicheki simu nakuta ni saa kumbi na mbili na nusu nikasema dah leo nimechelewa sana ikumbukwe nilikuwa na miadi ya kukutana na jamaa mmoja ni fundi mwezangu tulikuwa tuna deal la kwenda kufanya wote na aliniambia inabidi tukutane saa kumi na mbili sasa nikasema nimpigie simu nimepiga akapokea akaniambia mimi nishaondoka nishafika majohe alinigombeza sana unajua ilibidi niongozane nae majohe kulikuwa na deal la kujenga chuo kwa bwana flani

Sasa fundi mkuu akanifokea sana akasema kwa leo dili umelishindwa alinigombeza sana akasema kashatafuta mtu mwingine dah nikabaki mnyonge sana basi nikakata simu nikawa natafakari nini cha kufanya wakati nipo natafakari cha kufanya ghafla simu yangu ikaita kucheki namba ngeni nikajua labda fundi mkuu kabadili mawazo ikabidi niipokee haraka haraka hallow ile nimepokea nakutana na sauti nzuri ya kike hallow kaka mpolee mambo vipi?

Nikamwambia safi nani maana namba ngeni akanijibu mimi yule dada ulienisaidia jana kwenye gari mimi fatmah nikamjibu huku nikitabasamu wooow ww mdada jana nimekuota umekuja kwangu, akacheka sana akaniuliza kwani unataka kuniona kwa leo? Swali lake lilinipa furaha nikamwambia ndio kama vipi leo njoo kwangu japo sijui unaishi maeneo gani? Akanipa jibu lililonishangaza mimi nipo mtaa x hapo naishi kwa dadaangu anaitwa sakina jibu lililonishangaza sana itaendeleeaa........... leo jini wakuu nipo job hapa kidogo ila jioni naendelea japo itachukua wiki moja kuimaliza huu mkasa uliowahi kunikuta ni mkasa wa kweli.


Muendelezo bonyeza link hapo chini>>>

Sehemu ya pili

Sehemu ya tatu

Sehemu ya nne

Sehemu ya Tano

Sehemu ya Sita

Sehemu ya Saba
 
Back
Top Bottom