Mungu amewazungumzia majini kwenye kitabu kitakatifu cha Quran pale alipoelezea maisha ya Nabii Mfalme Suleyman bin Daud, wazungu wanamuita King Solomon.Kuwa Majini ni mafundi wajenzi wakubwa sana na pia ni wasanifu ktk kuunda!
Mfalme Suleyman alipewa uwezo na Mungu kuwatumia hawa kumsaidia kufanya kazi ktk maisha yake na walimjengea miundo mbinu mikubwa mno ktk ustawi wa Ufalme wake, Majengo makubwa yakiwemo Makasri ya mfalme Suleyman yalijengwa na majini .Yana uwezo wa kupiga kazi usiku na mchana mfululizo, pia ni great Divers (Wazamiaji) walimsaidia kumletea vito vingi vya thamani kutoka chini kabisa ya bahari ambapo mwanadamu hawezi kufika.Pia idadi yao ni kubwa kuliko sisi wanaadamu.
Majini wana uwezo wa kuishi miaka mingi zaidi ya mwanadamu, infact anaweza akashuhudi vizazi vyako hata vitano baada ya wewe kuondoka hapa ulimwenguni. Maskani yao kubwa ni baharini, ndio ..hii bahari tunayoiona ndani yake ina miji,majumba na kila kitu kama tunavyoishi sisi ktk mgongo wa ardhi, Majini yana uwezo wa kusafiri kwa kasi ya kufumba na kufumbua jicho ameshakwenda na kurudi mahala anapopataka. Wana uwezo wa kupaa angani na wengine wanaishi ardhini kwenye mgongo wa ardhi, kwenye misitu mikubwa na wengine wanaishi ndani ya ardhi chini kwenye mapango marefu.
Pia wana milki aka falme na koo kama tulivyosisi huku dunia.Kuna koo zao nyingine zina nguvu, zinaogopeka kwa nguvu na utajiri na nyingine ni za kawaida. Pia katika ulimwengu wao wapo walioasi yaani wabaya na hawa huitwa MASHETANI na pia wapo WEMA. Kiuhalisia Jini anatakiwa aishi maisha yake asimuingilie mwanadamu ktk kufanya maamuzi au kumahurutisha ktk maisha yake maana Mungu hajaumba nafsi mbili ktk kiwiliwili kimoja. So kitendo cha kumkalia mwanadamu ktk mwili wake kama kumfosi kimapenzi au kumfosi awe mganga au mchawi huku kunatafsirika kama UASI na jini huyo anabadilika na kuwa Shetani, na hapo inabidi atolewe kinguvu ili asiyaharibu maisha ya mwanadamu huyo.