Lycaon pictus
JF-Expert Member
- Jan 31, 2021
- 9,189
- 16,128
Ni miaka mingi iliyopita wakati nachukua kozi ya unesi chuo cha Muhimbili. Hosteli zipo karibu na taasisi ya MoI. Sasa nyuma ya Hosteli kuna barabara ambayo nilikuwa naenda kukimbia muda wa jioni saa moja hivi. Na huko nyuma kuna sehemu watu wa MoI huweka mazaga yao kama vitanda vibovu nk.
Kumbe wezi kutoka Magomeni huwa wanavuka mto Msimbazi na kuruka ukuta wa Muhimbili kuja kuiba vitu hivyo. Hivyo MoI wakawa wanaweka walinzi hiyo sehemu.
Siku hiyo jioni saa moja nakimbia jogging, naenda na kurudi. Ghafla nashangaa walinzi wawili wananifukuza kwa kasi nyuma yangu kimyakimya. Ile kuwaona nikasimama kuwaangalia wanakimbilia nini. Nao wakasimama, nafikiri wanajiuliza mwizi gani anasimama kutusubiria. Wakaniuliza unaenda wapi, ndiyo kuwaambia napiga tizi ni mwanafunzi wa unesi. Ndiyo wakanisimulia wanavyoibiwaga.
Pengine nisingewaona ningekula mtama kutokea nyuma. Unawaletea mazeozi wabongo!!