Siku Rais wa nchi akianzisha wadhifa wa Mfalme au Malikia na akamteua mkewe au mumewe kuwa Mfalne/ Malkia, si pia atakuwa sahihi?

Siku Rais wa nchi akianzisha wadhifa wa Mfalme au Malikia na akamteua mkewe au mumewe kuwa Mfalne/ Malkia, si pia atakuwa sahihi?

Salary Slip

Platinum Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
49,390
Reaction score
152,301
Kama Raia wa nchi anaweza kuanzisha ofisi yoyote na ikawa halali kikatiba, vipi siku Rais akiamua kuanzisha wadhifa wa Mfalme au Malikia na akamteua mwenza wake au mtu mwingine yoyote yule kushika wadhifa huo, si pia atakuwa sahihi?

Hata kama Katiba yetu inatambua Tanzania sio nchi ya kifalme (kwanza sijui kama katiba iko wazi kuhusu hili) lakini kama Katiba hiyo hiyo inampa madaraka ya kuanzisha ofisini yoyote, hapa. itakuwaje?

Kama anaweza kuanzisha cheo chochote, basi alikuwa sahihi kumtuma mwanae kwenda kuonana na Museveni nchini Uganda huku mwanae akiwa kiongozi wa timu(ofisi/cheo kipya).

Madaraka ya Rais wa nchi hii, ni bomu linalosubiri kulipuka siku moja.
 
Ndege ya Rais safari za Dubai yarudi na dolari za kubebwa na forklift truck. Kizimkazi festival ni DP World siyo hela ya kodi
 
Itakuwa ni DP World kupitia mgongo wa TPA ambao ni wafadhili halisi wa ujenzi wa kiwanja cha michezo huko Kizimkazi. Maana haingii akilini TPA wakajenge kiwanja cha michezo Zanzibar kwa hela za kodi tulizokamuliwa Watanganyika from no where.
 
Mkuu Salary Slip kwa ukongwe wako hapa JF, wengi hatukutegemea kama ungeweza kukaa chini na kuja na mada yenye swali au maswali ya namna hii.
 
Hata wakiteua marehemu au majini shega tu.
 
Kwa katiba yetu rais anaweza kuanzisha wizara ya kumtunza mume au mkewe.
 
Sidhani kama anaweza kuanzisha cheo cha juu kuliko chake. Maana akianzisha ufalme automatically urais utakuwa umekufa inabaki PM.
 
Mpaka hapa tu kwa nchi yetu Rais ni Mfalme! Yuko juu ya Katiba na Sheria!
Anaweza akamchagua mtu ye yote bila kuhojiwa wala kupingwa!
 
Kwa katiba yetu rais anaweza kuanzisha wizara ya kumtunza mume au mkewe.
Yes; kwa Katiba hii ana uwezo kabisa wa kufanya hivyo na chawa watatetea kwa hoja za kishamba bila hata aibu.
 
Mpaka hapa tu kwa nchi yetu Rais ni Mfalme! Yuko juu ya Katiba na Sheria!
Anaweza akamchagua mtu ye yote bila kuhojiwa wala kupingwa!
You're right! Urais wa Tanzania kwa mamlaka hauna tofauti na ufalme tena absolute monarchy kama wa KSA na sio constitutional monarchy kama ule wa UK.
 
Kama Raia wa nchi anaweza kuanzisha ofisi yoyote na ikawa halali kikatiba, vipi siku Rais akiamua kuanzisha wadhifa wa Mfalme au Malikia na akamteua mwenza wake au mtu mwingine yoyote yule kushika wadhifa huo, si pia atakuwa sahihi?

Hata kama Katiba yetu inatambua Tanzania sio nchi ya kifalme (kwanza sijui kama katiba iko wazi kuhusu hili) lakini kama Katiba hiyo hiyo inampa madaraka ya kuanzisha ofisini yoyote, hapa. itakuwaje?

Kama anaweza kuanzisha cheo chochote, basi alikuwa sahihi kumtuma mwanae kwenda kuonana na Museveni nchini Uganda huku mwanae akiwa kiongozi wa timu(ofisi/cheo kipya).

Madaraka ya Rais wa nchi hii, ni bomu linalosubiri kulipuka siku moja.
Kwa hali ilivyo yawezekana hata sasa tupo kwenye utawala wa kisultan
 
Kama inawezekana nyumbani kwako ukapeleka mtu mwingine na kuwaambia wanao kwamba huyu ndio baba yenu kuanzia leo, basi hapo sawa, lakini kama hiwezekani basi na rais hivyo hivyo hawaezi kuchagua mtu akawe juu yake
Haijalishi ni mama au baba

Mwacheni mama apige kazi
Matunda mtayaona tu
 
Ufalme au Umalkia utakuwa na maana gani ikiwa ni wa kuteuliwa? Atabaki na ataendelea kuwa mteuliwa na mamlaka yake ya uteuzi itakuwa ni Rais

Leteni hoja zenye mashiko tuzidadavue sio haya malonyalonya.
 
Back
Top Bottom