Kiwalani finest
Member
- Jul 6, 2024
- 97
- 72
SIKU TUKIWEKA PEMBENI UJINGA WA KULINDANA
Tukalimana kwa mujibu wa ilani, katiba, kanuni, miongozo na taratibu, na tukaazimia kutenda haki bila kuwaonea mafukara, tukausaka usawa — siku hiyo itabarikiwa na kuifanya nchi ineeemeke kwa haki.
Nilisikika huko ndotoni nikitema cheche, nikikemea tabia mbovu na chafu zinazonuka uvundo zinazoshamiri za kuwalinda viongozi wanaodharau sauti za mafukara zinapopazwa.
Nikaamua kupeleka moto. Nakumbuka tarehe 26/09/2022, Bi Leila Mavika, Mkurugenzi wa Maadili, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, alisema: "Utu na ustaarabu ni kuheshimu sheria. Ndiyo haya maadili tunayoizungumzia. Kuheshimu sheria zinazoongoza nchi kwa ujumla wake, sheria ambazo zinaongoza taasisi mbalimbali — vyote hivyo tunapaswa kuheshimu." Mwisho wa kunukuu.
Heshima ya kiongozi yeyote, awe wa chama cha siasa au wa serikali, jambo la kipaumbele kwake la kwanza kabisa ni kuipa uzito Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 1977, toleo la 2005, ibara 26(1)(2), ibara 09(a,b,f,h) na ibara 29(1)(2). Mheshimiwa Dkt. Eliezeli Mbuki Feleshi, Ex Mwanasheria Mkuu wa Serikali, akifanya mahojiano na ITV, nakumbuka tarehe 29/08/2022, alisema: "Sheria ikishatungwa, kinachofuata sasa ni kila mtu kuiishi na kufuata sheria. Katiba (ya nchi) ndiyo sheria mama." Mwisho wa kunukuu.
Maneno yanajitosheleza; hayahitaji ufafanuzi. Baada ya hapo, ni kiongozi kujipanga katika maisha yake yote ya uongozi kuishi akiisujudia ibara 08(1)(a,b,c,d) ya katiba, kwa uwezo wa sala anazosali kwa Mwenyezi Mungu kwa mujibu wa imani yake ya kidini. Kiongozi hapaswi kuwa mtu mwenye dharau, mwenye kutamka maneno kwa hila au kuonyesha matendo ya kibaguzi yanayopelekea walio chini yake kuamini kuwa ni mla rushwa. Steven Masato Wasira, mwanasiasa mkongwe, akifanya mahojiano na Mwanahabari, nakumbuka tarehe 18/10/2021, alisema: "Rushwa ni problem kwa maendeleo, sio tu ya Tanzania, bali ni problem kwa dunia nzima." Mwisho wa kunukuu.
Wasaliti namba moja ndani ya CCM ni viongozi wala rushwa, ambao wamejaa dharau na hawasikilizi sauti ya wanyonge, huku tukijinasibu kuwa sisi ni chama cha kutetea wanyonge. Viongozi wa kitaifa wakisema neno, huku chini kuna baadhi ya viongozi walio madarakani, waliowekwa na wakubwa, ambao hawajali wala kuzihofu sauti za viongozi wa kitaifa. Nakumbuka tarehe 06/10/2024, Comrade Dkt. Emmanuel John Nchimbi, Katibu Mkuu wa CCM Taifa, alisema: "CCM ni chama ambacho kimeendelea kushika misingi yake kwamba hiki ni chama cha wanyonge, chama kinachotetea maslahi ya watu." Mwisho wa kunukuu.
Tunao viongozi waliojawa na dharau ya kuwadharau mafukara, ambao hata wapaze sauti vipi, wao wanakuwa na kazi ya kumlinda kiongozi anayenuka badala ya kukaa na wanachama na kuwasikiliza. Wanatumia ubabe na kauli za vitisho kuwakebehi wanaoonyesha maovu. Viongozi hao, wabeba maovu, wana hasira muda wote na hawamini katika katiba ya CCM 1977 toleo la 2022, ibara ya 15(7), ambayo inasema kuwa kukosoa na kukosolewa ni sehemu ya wajibu wa kila mwanachama.
Mheshimiwa Steaven Masato Wasira, Ex Waziri na Mwenyekiti wa Chuo cha Kivukoni, akifanya mahojiano na Mwanahabari Odemba, nakumbuka tarehe 18/10/2021, alisema: "Mimi sielewi kama wako viongozi ambao hawataki kukosolewa. Kama wapo, ni bahati mbaya." Mwisho wa kunukuu.
Kama kweli tunataka kuisaidia nchi kusonga mbele, turudi kwenye maandiko yetu. Tuache kujenga uswahiba na kuchukua hatua kwa mitazamo ya cheo cha mtu. Tutende haki na usawa. Viongozi wanaosemeka vibaya ndani ya jamii, walio na dharau, watoke tu.
Tunao vijana wengi ndani ya CCM, wenye elimu zao na utii, ila hawana godfather wa kuwapigia chapuo kutokana na uchawa ulioota mizizi unaolindwa kwa nguvu zote. Mheshimiwa Mizengo Kayanza Peter Pinda, Mtoto wa Mkulima, Ex Waziri Mkuu, akifanya mahojiano na Mwanahabari, nakumbuka tarehe 18/07/2020, alisema: "Sasa hivi hatuna uhaba wa vijana makada wasomi wa kweli." Mwisho wa kunukuu.
Tuheshimu kauli za viongozi wetu wakuu. Hatuna sababu za kuwakumbatia viongozi wenye uelewa duni kisa tuna enjoy fedha zao za rushwa wanazotupatia ili tuwalinde, huku tukijua sisi viongozi tuna dhima ya kuhifadhi, kulinda, na kutetea katiba na sheria za nchi kwa mujibu wa ibara 26(1)(2) na ibara 09(a,b,f,h) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 1977 toleo la 2005.
Jaji Dkt. Eliezeli Mbuki Feleshi, Ex Mwanasheria Mkuu wa Serikali, akifanya mahojiano na ITV, nakumbuka tarehe 29/08/2022, alisema: "Watu wanafuata sheria na tunaheshimu watu wafuate sheria. Kwa sababu nchi yetu inaongozwa kwa mujibu wa sheria. Watu wasipofuata sheria, tutaendelea kuhakikisha kwamba tunawaelimisha wafuate sheria." Mwisho wa kunukuu.
Nikashtuka katika ulimwengu wa kiroho huko ndotoni, nikiwa kimya.
Kidumu Chama cha Mapinduzi
Mathias Mugerwa Kahinga