Wala usihangaike Yesu ndiye njia, kweli, na uzima. Wachawi wenyewe wanakiri wazi kuwa nguvu zao hufifia mbele ya jina la Yesu. Hakika, jina la Yesu lina mamlaka juu ya kila giza, hofu, na minyororo ya kiroho.
Ukiwa umelemewa, umehangaika, au umezunguka kila kona bila msaada wa kweli leo ni siku yako ya wokovu. Hili ndilo tumaini kuu: hata kama maisha ya baada ya kifo ni fumbo kwa wengi, Yesu ndiye Nuru wa ukweli na uzima wa milele. Usikawie. Fungua moyo wako sasa.
Naomba nikuongoze Sala ya Toba.
Sema Bwana Yesu
Ninakuja mbele zako nikiwa mnyenyekevu, nikiwa nimelemewa na uzito wa maisha haya na maswali ya maisha yajayo.
Najua siku nitakayokufa ndipo nitakapojua ukweli kamili kuhusu hatma yangu, lakini leo hii, kabla hiyo siku haijafika, natamani nikuamini wewe na nikupe moyo wangu wote.
Bwana Yesu,
Ninakuamini kama Njia, Kweli, na Uzima.
Ninakiri kwamba mimi ni mwenye dhambi,
Nimeishi maisha yangu mbali na wewe.
Leo ninarudi kwako.
Naamini kwamba uliteswa, ukafa kwa ajili yangu, na siku ya tatu ukafufuka kwa ushindi.
Nakupokea kwa moyo wangu wote kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yangu.
Nisamehe dhambi zangu zote, nisafishe kwa damu yako takatifu.
Nifanye kiumbe kipya.
Andika jina langu katika Kitabu cha Uzima.
Niongoze kila siku, hadi nitakapokutana nawe uso kwa uso.
Nijaze na Roho Mtakatifu, unifunze kutembea katika mapenzi yako.
Leo hii ninajisalimisha kwako kwa imani, si kwa kuona
Naamini kuwa wewe ndiye tumaini la kweli,
Na maisha yangu mapya yanaanza sasa ndani yako.
Asante kwa kunipenda, kunisamehe, na kunipokea.
Katika jina la Yesu, Amina.
Kama umeomba sala hii kwa moyo wa kweli, hongera umefanya uamuzi wa milele.
Karibu katika familia ya Mungu. Tafuta kanisa linalohubiri Neno la Mungu kwa kweli, soma Biblia kila siku, na tembea na Yesu katika kila hatua.
Yesu anakupenda, na maisha yako hayatabaki kama yalivyokuwa tena.