Siku tutakayokufa ndio tutaujua Ukweli kuhusu hatma yetu baada ya kifo

Siku tutakayokufa ndio tutaujua Ukweli kuhusu hatma yetu baada ya kifo

Ukifa umekufa tu kama kuku anavyokufa ndivyo nabinadamu hufa , ila sio vibya kuamini kwa kujifariji tu
 
Una hakika gani na hilo?
Au na wewe unaimani tu?
Naamini kitu gani wewe huoni kuwa mtu akifa amekufa hasikii , mfumo wa fahamu wote unasimama wala hapatiani popote zaidi ya mwili wake kuanza mchakato wa kuooza? Hapo unahitaji uhakika up
 
Sisi Waislamu tunajua kua kuna maisha baada ya kifo na malipo ya maisha uloishi hapa duniani yapo

Kwaio kma ww hujui sawa ila ss waislamu tunajua kua kuna maisha baada ya kifo
 
2050 Nadhani 🆔 yangu itakuwa inasoma RIP
Usijitamkie hivyo. Miaka 25 tu ijayo naamini bado utakuwepo mkuu japo haisaidii cho chote maana hata kama tungeishi miaka 10,000 ni kazi bure!
 
Kila nikitafakari sana kuhusu hili swala la maisha baada ya kifo katika Angle ya hizi dini zetu nagundua sisi wanadamu hatujui hatma yetu baada ya maisha haya. Muislamu anasema hili mkristo anasema lake...wa budhaa nao wanasema kivyao ,wahindu nao vilevile wanaelezea maisha ya kifo wanavyojua wao ilimradi tu changanyikeni...

Yaani hatuna uhakika kuhusu afterlife... anyway kama kuna mbingu au jehanamu au tutaingia kwenye dimension nyingine tofauti na hii tuliyopo , basi itajulikana tu siku ile tu tutakapokufa.

Mshana Jr
Kwa Elimu yangu nahitimisha kuwa maidha baada ya kufa ni sawa na maisha kabla hujazaliwa.
Full stop.
 
Tupo ndani ya Kristo, ambako hawezi kututoa. Tukipotea hapa duniani tutakuwa tunaishi alipo yeye(Kristo)
 
Wala usihangaike Yesu ndiye njia, kweli, na uzima. Wachawi wenyewe wanakiri wazi kuwa nguvu zao hufifia mbele ya jina la Yesu. Hakika, jina la Yesu lina mamlaka juu ya kila giza, hofu, na minyororo ya kiroho.

Ukiwa umelemewa, umehangaika, au umezunguka kila kona bila msaada wa kweli leo ni siku yako ya wokovu. Hili ndilo tumaini kuu: hata kama maisha ya baada ya kifo ni fumbo kwa wengi, Yesu ndiye Nuru wa ukweli na uzima wa milele. Usikawie. Fungua moyo wako sasa.

Naomba nikuongoze Sala ya Toba.

Sema Bwana Yesu
Ninakuja mbele zako nikiwa mnyenyekevu, nikiwa nimelemewa na uzito wa maisha haya na maswali ya maisha yajayo.
Najua siku nitakayokufa ndipo nitakapojua ukweli kamili kuhusu hatma yangu, lakini leo hii, kabla hiyo siku haijafika, natamani nikuamini wewe na nikupe moyo wangu wote.

Bwana Yesu,
Ninakuamini kama Njia, Kweli, na Uzima.
Ninakiri kwamba mimi ni mwenye dhambi,
Nimeishi maisha yangu mbali na wewe.
Leo ninarudi kwako.
Naamini kwamba uliteswa, ukafa kwa ajili yangu, na siku ya tatu ukafufuka kwa ushindi.

Nakupokea kwa moyo wangu wote kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yangu.
Nisamehe dhambi zangu zote, nisafishe kwa damu yako takatifu.
Nifanye kiumbe kipya.
Andika jina langu katika Kitabu cha Uzima.
Niongoze kila siku, hadi nitakapokutana nawe uso kwa uso.
Nijaze na Roho Mtakatifu, unifunze kutembea katika mapenzi yako.

Leo hii ninajisalimisha kwako kwa imani, si kwa kuona
Naamini kuwa wewe ndiye tumaini la kweli,
Na maisha yangu mapya yanaanza sasa ndani yako.
Asante kwa kunipenda, kunisamehe, na kunipokea.
Katika jina la Yesu, Amina.

Kama umeomba sala hii kwa moyo wa kweli, hongera umefanya uamuzi wa milele.
Karibu katika familia ya Mungu. Tafuta kanisa linalohubiri Neno la Mungu kwa kweli, soma Biblia kila siku, na tembea na Yesu katika kila hatua.
Yesu anakupenda, na maisha yako hayatabaki kama yalivyokuwa tena.
 
Maisha baada ya kifo yapo, kumbuka tajiri na lazaro (Luka 16:19-13). Uhalisia ni kwamba kinachokufa ni mwili wako tu, lakini wewe haufi kinachotokea tunahamishwa kutokwa kwenye mwili huu wa duniani tunapewa mwili mpya, huu mwili ni vazi tu tulilovalishwa, kwa hiyo ukifa akili yako itakuwepo, ufahamu wako utakuwepo, hisia zitakuwepo. tusijidanganye kusema mtu akifa anakufa tu kama kuku, mwili wako unakufa ila nafsi yako na roho yako vitakuwa hali milele.
 
Usijitamkie hivyo. Miaka 25 tu ijayo naamini bado utakuwepo mkuu japo haisaidii cho chote maana hata kama tungeishi miaka 10,000 ni kazi bure!
Amina mkuu
 
Ukifa umekufa hutojua umekufa na hakutakuwa na kitu au hisia zozote.
 
Back
Top Bottom