KING MIDAS
JF-Expert Member
- Dec 1, 2010
- 8,589
- 16,936
Kipindi cha mashindano ya dunia kule Budapest, Hungary; Anita Alvarez alizama chini kabisa mwa Pool.
Ukiangalia pale kwenye dawati la wakufunzi, Andrea Fuantes ambaye ni kocha wake anaonekekana kutokuwa na utulivu sababu mwanafunzi wake yupo chini kwa muda mrefu.
Anakurupuka na kuzama majini kama alivo bila kujali kavaa nini, alimnyakua na kumtoa hadi sehemu salama.
Kwa muda huo Anita alikuwa hana fahamu na asingeweza kujitoa ndani ya maji kwenye kile kina.
Isingekuwa Andrea kutambua lile angekufa ndani ya maji. Kwakuwa alikuwa anamtazama ilikuwa rahisi kutambua kuwa kulikuwa na tatizo ndio mana alielewa amekaa kwa muda na mtefu na kufanya maamuzi ya ghafla bila kufikiria mara mbili.
Unapokuwa chini kwa muda mrefu, akina nani huweza kutambua kwa haraka uko ndani ya tatizo? Ambao watakuja kukutoa nje ya magumu yako pale unapokosa nguvu zako binafsi kujinasua?
Yupo anayekutegemea siku akijikuta kazama ndani ya shimo wewe utamtafuta na kumvuta kutoka ndani ya giza kwa muda mrefu? Ujitose kwaajili yao kwa kukosa tena nguvu za mapambano juu ya haya maisha?
Mungu ameliweka jina lako katika masikio ya mtu fulani ambaye anaweza badili maisha yako.
Tafakari kwa undani 👑