Siku Viongozi Wakuu wa Serikali wakifanya haya nitaamini ni Wazalendo

Siku Viongozi Wakuu wa Serikali wakifanya haya nitaamini ni Wazalendo

kifupi kirefu

JF-Expert Member
Joined
Oct 29, 2018
Posts
539
Reaction score
3,507
1. Wakiacha kujilipa mishahara mikubwa na posho za vikao na safari, kisha kuelekeza fedha walizostahili zikatengeneze huduma za kijamii. Hakuna ukweli kwamba wao wanalipiwa nyumba, posho, mishahara na marupu rupu kibao then tuwaite wazalendo. Wao wanakula zaidi kuliko sisi?

2. Siku watoto wao wakianza kusoma shule na vyuo vya serikali. Kama wanaamini elimu yetu ni Bora kwanini watoto wao hawasomi kwenye Shule za Serikali? Uzalendo wao upo midomoni si kwenye matendo, wafanye tujue wapo na sisi.

3. Watakapo ondoa kinga ya kushtakiwa. Kama wanajiamini ni wazalendo na wanatutendea mema Basi waondoe kinga yakuishtakiwa ili wanapobainika kutumia madaraka vibaya au kutuibia washtakiwe. Leo hii wanajimilikisha na kutenda Mambo ya Jinai wanavyojisikia wakiamini Wana kinga. Huu uzalendo wa aina gani?

4. Siku wakiacha tu kujiita waheshimiwa yaani wakajiondolea utukufu na kujishusha kuwa ndugu kwetu. Wameshindwa kufanya 1-4 wafanye Basi hata ili dogo lakujiondolea utukufu.

Kama hawafanyi haya ni vigumu kutuambia wao ni viongozi wa wanyonge. Hakuna wanyonge wenye sifa hizi. Kidumu chama Cha tuwanyonge.
 
Back
Top Bottom