Siku watu wakikutana watakimbiana humu!

Mimi naomba uniondoe kwenye kundi hili, kwa sababu hata kiwaja sina! Vile vile sijawahi kudai madai yoyote ya aina hiyo, ni mtoto wa mkulima sawa na Mh. Pinda tu!
Nyinyi ndo vigogo mnaficha mali
 
We unampango wa kishushushu. Yule mwenye ile I'd fulani anatoka ofisini ya mkulu, na amekuwa akitunyetisha zile issue nyeti za kule. Unadhani atakuja humo? Umetumwa?
 
Nyinyi ndo vigogo mnaficha mali
Ukiwa umeficha mali huwezi tena ukawa na ujasiri wa kujitetea kwenye mitandao. Ukifanya hivyo utakuwa unafanya kosa kubwa mno na la makusudi ya kuipa kazi serikali, maana utakuwa unaisababisha ianze kujiuliza maswali, HAPA KUNA NINI? Katika maisha yako yote, epuka kitu kuisababisha Serikali ikufanyie kazi, nadhani ni kati ya vitu vigumu karibia kuzidi vyote hapa duniani. Ussipe kazi Serikali, acha yenyewe ikupe kazi kama inaona unafaa!
 
Mwacheni anatoa Stress...maana kwa sasa unakuwa na mahasira yako rohoni huoni pa kubwagia.Ukizibwaga hovyo hovyo kesho kirobani coco ufwukeni mara ume disapia kama moshi wa kumchagua papa kule Roma.Bora ametoa ya rohoni,nafsi imemtulia pasipo wasi.JF ina kila aina wa watu,makapuku,wabeba box,wang'oa kucha.Kifo cha mende,Forex,qnet,wauza kuku,mama ntili,Humu ni zaidi ya mtaa unaoujua.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…