Siku watu wakikutana watakimbiana humu!

Siku watu wakikutana watakimbiana humu!

Mbona wengine wanafahamiana humu na maisha yao yana uhalisia wa kweli and then some?

Si kila mtu humu muongo. Nashukuru Mungu wale niliowaamini humu na wao kuniamini humu walikuwa wakweli 110%

Kwa maisha tunayoishi jf ya ufahari mkubwa
Magari ya bei mbaya!

Majumba ya kifahari

Kazi nzuri nzuri

Mavazi ya kifahari
Jf hakuna aliyepanga chumba kimoja labda Nyumba nzima kodi 3 millions na zaidi

Hakuna anayekula kwa shida!

Kila mtu anatembea amekaa tena sio starlet!

Hakuna anayepata mshahara Wa chini ya laki 9!
Wote tumeajiriwa vitengo nyeti!
Au tuna mabusiness au makampuni cc husnathebossylady!

Hakuna anayeungaunga life!

Wote tuko mahandsome na mabeautifu
Tuna ngozi nyororo na sura za mvuto!

Mods naomba watusaidie kupanga get together party walau tukutane one day!
Na wamikoani nao waje dar! Au Wa dar waende mikoani
 
Thread ya uongo sana hii,
Jf wengi ni wa wazi hata thread za watu kushindia karanga utazipa humu.
Jf kumejaa wapangaji sana.
Jf kumejaa watafuta kazi hadi za laki na hamsini.
Jf hakuna instag life.
Jf kuna watu wa vitengo ila ni kwa siri kubwa,wanaojisema ni wanogeshaji mada tu.
 
Back
Top Bottom