JamiiForums
JF Official Account
- Nov 9, 2006
- 6,249
- 5,747
Baadhi ya wageni
Msanii Vitalisi Maembe akitoa burudani
Maadhimisho hayo yalianza na mbio za Kilometa Tano “Fun Run” zilizoanzia kwenye Viwanja vya Ghymkana / Mgambo na kuhitimishwa katika eneo hilo na kushirikisha Wadau mbalimbali siku ya 1 April 27, 2025
Maadhimisho hayo yanaratibiwa na JamiiAfrica, Serikali, Shirika la Kimataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO) pamoja na Wadau wengine wa Habari ndani na nje ya Tanzania. Kaulimbiu ya mwaka huu, “Uhabarishaji katika Dunia Mpya: Mchango wa Akili Mnemba kwenye Uhuru wa Vyombo vya Habari,”
Hotuba ya Maxence Melo, Mkurugenzi Mtendaji, JamiiAfrica
Katika dunia ya sasa, vyombo vya habari havihusishi tena magazeti, redio na televisheni pekee kama zamani. Tunashuhudia kuongezeka kwa watengeneza maudhui wa dijitali ikijumuisha wanablogu, wapiga picha huru, vloggers, podcasters na wengine wengi ambao, kwa ubunifu wao, wamepanua mipaka ya uhuru wa kujieleza.
Tunatambua mchango wao mkubwa katika kuweka jamii zetu hai kwa taarifa, fikra na mazungumzo muhimu. Tunasisitiza kuwa uhuru wa habari lazima uwe shirikishi, ukilinda na kuenzi haki za makundi yote yanayochangia katika mnyororo wa mawasiliano ya kisasa
Kaulimbiu ya Mwaka 2025
Kaulimbiu ya mwaka huu, “Uhabarishaji katika Dunia Mpya: Mchango wa Akili Mnemba kwenye Uhuru wa Vyombo vya Habari,” inatukumbusha kwamba katika nyakati hizi za taarifa nyingi na teknolojia za kisasa, tunahitaji uwezo wa ziada kuchuja, kuchambua, na kuelewa taarifa kwa umakini wa hali ya juu ili kulinda uhuru wetu wa habari na kuhakikisha uwajibikaji wa wale wanaohabarisha na wale wanaohabarishwa(Informer na wale wanaokuwa informed)
Umuhimu wa Akili Mnemba
Katika mazingira haya mapya, akili mnemba (undwe) imekuwa nyenzo isiyokwepeka katika tasnia ya habari na uchakataji taarifa. Wanahabari na jamiikwa ujumla (watumiaji wa habari) wanahimizwa kuwa na uwezo wa kuchambuachanzo cha taarifa na kutambua upendeleo au propaganda zinazoweza kuathirimaudhui.
Ripoti ya UNESCO 2023
Kwa mujibu wa ripoti ya UNESCO ya mwaka 2023 kuhusu Uhuru waVyombo vya Habari, "Uwezo wa kupima ubora wa taarifa ni ujuzi muhimu kwa kilamtu katika karne ya ishirini na moja." Hii inaonyesha kuwa, si vyombo vya habari pekee vinavyopaswa kuwa na viwango vya juu vya weledi, bali pia jamii inapaswa kujifunza jinsi ya kuwa wasomaji, watazamaji na wasikilizaji makini.
Mabadiliko ya Teknolojia
Tasnia ya habari, ikiwa kwenye mabadiliko makubwa yanayosukumwa namaendeleo ya teknolojia, inahitaji kuwekeza zaidi katika kukuza uelewa wateknolojia zinazoibukia (emerging technologies) na hasa matumizi ya akilimnemba kwa wanahabari wake. Katika nyakati hizi, kuimarisha akili mnemba si tuhitaji la mtu binafsi, bali ni jukumu la pamoja kwa tasnia ya habari na jamii nzima. Uhuru wa vyombo vya habari unapata maana kamili pale unapochanganyika nauwajibikaji, uchambuzi wa kina na uelewa sahihi wa taarifa zinazochakatwa.
Uhuru wa Vyombo vya Habari na Uchaguzi Mkuu
Kadhalika, tunapotazama mbele kuelekea Uchaguzi Mkuu, hatuna budi kuangaziakwa umakini zaidi mazingira ya kazi za waandishi wa habari na watengenezamaudhui. Ni katika nyakati kama hizi ambapo uhuru wa habari hupimwa kwa vitendo – si kwa maneno matupu. Tunatoa wito kwa mamlaka, taasisi, vyama vya siasa na jamii kwa ujumla kuheshimu na kulinda uhuru wa vyombo vya habari,kuhakikisha kuwa hakuna vitisho, mashinikizo wala vizingiti vinavyowekwa kwawanaohakikisha wananchi wanapata taarifa sahihi, za kina na kwa wakati.
Uhuru wa Vyombo vya Habari ni Haki, si Hisani
Ni wajibu wa kila mmoja kulinda uhuru wa habari kila siku – wanahabari, raia, watunga sera na wanateknolojia.
Neno la Shukrani
Tunatoa shukrani nyingi kwa Mashirika ya Kimataifa na wadau wote wa maendeleo kwa kuendelea kusimama nasi katika safari hii ya kuhakikisha uhuru wa habari unalindwa na kuenziwa
Kwa heshima na furaha kubwa, naomba nianze kwa kuishukuru UNESCO, Serikali ya Tanzania na JamiiAfrica kwa kuandaa tukio hili muhimu. Mmefanya kazi ya kupigiwa mfano.
Ni heshima kubwa kwangu kuwa hapa leo kushiriki nanyi katika maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani 2025. Siku hii ni fursa ya kusherehekea mchango wa vyombo huru vya habari, lakini pia kutafakari changamoto zinazowakumba waandishi wa habari, hasa katika dunia inayobadilishwa na Akili Bandia (AI), taarifa potofu, na kupungua kwa nafasi ya ushiriki wa kiraia.
Mnamo mwaka 1766, Sweden iliweka historia kwa kuwa taifa la kwanza duniani kutangaza rasmi uhuru wa vyombo vya habari. Hatua hiyo ilianzisha zama mpya za kusimamia ukweli na uwazi. Leo hii, mazingira ya uandishi wa habari yamebadilika sana, huku teknolojia kama AI ikifungua fursa mpya na vilevile changamoto.
Akili Bandia: Fursa na Changamoto
Tukiangalia maendeleo ya AI, binafsi ninaiona kama jambo linalotia matumaini lakini pia linaloleta mashaka. AI inaweza kuwasaidia waandishi wa habari kufanya kazi kwa kasi zaidi, kuchambua taarifa nyingi na kufichua ukweli uliokuwa umefichika. Hata hivyo, AI pia inaweza kutumiwa vibaya kusambaza taarifa za uongo kama vile picha na video bandia, na maandiko ya kubuni. Hili ni suala la uaminifu zaidi kuliko teknolojia pekee.
Nchini Sweden, tunaelekeza maendeleo ya AI kwa kufuata misingi ya:
- Kulinda faragha na usalama wa taarifa za watu,
- Kuhakikisha uwazi wa matumizi ya AI,
- Kupambana na upendeleo na kuhakikisha usawa.
Uandishi wa Habari wa Ujasiri Barani Afrika
Nikiwa hapa Tanzania na Afrika kwa ujumla, nimevutiwa na ujasiri mkubwa wa waandishi wa habari. Licha ya changamoto kama ukosefu wa rasilimali, udhibiti, na vitisho, bado waandishi hawa wanapaza sauti zao kwa ajili ya haki.
Nilipowatembelea waandishi wa habari wa UTPC, niliona changamoto zao moja kwa moja kama ilivyotokea Manyara na Njombe, ambapo waandishi walihatarisha maisha yao kusimulia ukweli kuhusu ukatili wa kijinsia na watoto wenye ulemavu. Hadithi hizi zinathibitisha umuhimu wa kazi yetu.
Mwelekeo Mpya: Suluhisho za Ndani
Katika zama hizi za kidijitali, aina mpya ya ujasiri inahitajika. Waandishi wa habari wanapaswa kupambana na mashambulizi ya mtandaoni, ufuatiliaji wa siri, na taarifa potofu — lakini pia kutumia teknolojia kuwahabarisha na kuwahamasisha watu.
Majukwaa kama JamiiCheck yananipa matumaini. Hizi ni mbinu za ndani kupambana na changamoto za kidijitali. Kuviunga mkono ni kuijenga jamii yenye taarifa sahihi.
Uhuru wa Kujieleza: Nguzo ya Demokrasia
Kwanini uhuru wa kujieleza ni muhimu?
Tunaamini kuwa jamii hunufaika pale watu wanapopewa uhuru wa kuzungumza, kushiriki na kutofautiana. Hakuna mtu au chama chenye majibu yote. Tunahitaji majadiliano wazi kwa maendeleo.
Katika mfumo wa vyama vingi, uhuru wa habari huwasaidia wananchi kufanya maamuzi bora, huwawajibisha viongozi, na kuimarisha nafasi ya raia kushinikiza mabadiliko.
Kwa kila mwandishi wa habari aliye hapa leo na duniani kote — nawapongeza kwa ujasiri wenu. Mko mstari wa mbele kuandika mustakabali wa habari.
Endeleeni kusimulia hadithi zinazobadili maisha. Endeleeni kuuliza maswali yenye uzito. Endeleeni kuangaza nuru katika giza.
Mwakilishi wa UNESCO, Michael Toto
Leo tunapoadhimisha miaka 33 ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani, tunakumbushwa kuwa vita ya kulinda uhuru huu bado ni kubwa duniani kote. Mwaka huu, UNESCO imelaani mauaji ya zaidi ya waandishi wa habari 90 waliouawa kwa kusimamia ukweli kuanzia Ulaya hadi Afrika, Asia na Amerika Kusini.
Waandishi wa habari bado wanateseka kwa vitisho, manyanyaso na hata kuuawa, kwa sababu tu ya kufanya kazi yao ya msingi kuhabarisha kwa ukweli.
Siku hii inatufundisha kuwa kusema ukweli si kosa; uandishi wa habari ni nguzo ya demokrasia, uwajibikaji na amani. Ni wajibu wetu sote serikali, mashirika ya kimataifa, vyombo vya habari na wadau wa maendeleo kutafakari kwa kina Tumefanya nini? Tunapaswa kufanya nini zaidi?
Tunapaswa kuongeza msaada kwa waandishi wa habari, na kulinda uhuru wa kujieleza hasa sasa tunapokabili mapinduzi ya Akili Bandia (AI). AI inaleta fursa nyingi lakini pia inatishia haki na uhuru wetu, ikiibua maswali kuhusu ukweli, uaminifu, na mustakabali wa uandishi wa habari.
UNESCO itaendelea kushirikiana na serikali, jamii na vyombo vya habari kuhakikisha waandishi wanafanya kazi zao kwa usalama na uhuru katika zama hizi mpya za teknolojia.
Hotuba ya Jumuiya ya Afrika Mashariki
Tunalindaje Uhuru wa Vyombo vya Habari katika Dunia ya Akili Bandia?
Kwangu, hili si suala la sera tu, bali ni la binafsi. Kabla ya kuingia serikalini, nilihudumu zaidi ya miaka 10 kama mwandishi wa habari Afrika Mashariki. Wakati huo, watu walitegemea waandishi wa kitaaluma kupata taarifa sahihi. Teknolojia ya kidijitali ilikuwa inaanza, na imani kwa vyombo vya habari ilikuwa kubwa.
Leo, mambo yamebadilika sana. Uandishi wa raia umeongezeka, na Akili Bandia (AI) inabadilisha ukusanyaji na usambazaji wa habari. Licha ya fursa kubwa, tunakabiliwa na changamoto kama taarifa za uongo, kupungua kwa imani ya umma, na habari feki zinazotengenezwa na AI.
Changamoto yetu ni kutumia teknolojia mpya bila kupoteza misingi ya ukweli, uadilifu na uwazi katika uandishi wa habari.
Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) inalenga kutumia AI kwa maendeleo:
- Kupitia Mkakati wa Mabadiliko ya Kidijitali wa miaka mitano,
- Kwa msaada wa dola milioni 40 kuimarisha miundombinu ya kidijitali,
- Kujenga vituo vya data na ubunifu,
- Kuweka sheria za kulinda data,
- Na kutoa mafunzo ya ujuzi wa AI kwa zaidi ya wanafunzi 50,000 kupitia Kituo cha Umahiri cha ICT Arusha.
Kulinda uhuru wa vyombo vya habari katika zama za AI kunahitaji ushirikiano wa wadau wote.
Waandishi wa habari lazima washikilie maadili, serikali ziweke mifumo ya kulinda uhuru wa kujieleza, na wote tushirikiane kupambana na taarifa potofu.
Kwa pamoja, tunaweza kuhakikisha kuwa uandishi wa habari unabaki kuwa nguzo thabiti ya demokrasia, hata katika enzi ya Akili Bandia.
Picha: Wazungumzaji wakijadili kuhusu Athari za Akili Mnemba(AI) katika Mustakabali wa Uandishi wa Habari
Mkurugenzi Mtendaji wa JamiiAfrica, Maxence Melo, akizungumza katika mjadala unaohusu Athari za Akili Mnemba(AI) katika Mustakabali wa Uandishi wa Habari, amesema Wakati wa Uchaguzi Mkuu 2025 tutashuhudia Matumizi ya Kidigitali kwa kiwango cha juu kuliko wakati mwingine wowote Nchini ikiwemo matumizi ya AI ambayo tayari yalianza kutumika katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa. JamiiAfrica kwa kushirikiana na Wadau mbalimbali wakiwemo Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) tunawajengea uwezo Wadau wa Siasa kuhusu matumizi ya Digitali.
Mjadala : Testimonies from Journalists – Tech & AI’s Impact on Journalism
Danstan Kamanzi (TMF)
Ili waandishi waweze kuwa mbele kuendena na mabadiliko ya teknolojia kuboresha kazi zao wanahitaji mambo matatu
- Shauku ya kubadilika na kukua, kubadilisha sekta ya habari na jamii kwa ujumla
- Utayari wa ku-invest kwenye kujifunza na kutafuta ujuzi mpya
- Kudhamiria na kujikita kwenye majukumu yao (determination and focus.)
Ni muhimu kuzalisha maudhui kuendana na mahitaji ya jamii, hayo mengine wanaweza kuzalisha wenyewe.
Changamoto ambayo inatakiwa kufanyiwa kazi na Wanahabari ni kuangalia jinsi gani wanaweza kuitumia Akili Mnemba (AI) kuingiza kipato, kwa kuwa AI inazalisha taarifa ambazo zinalishwa na sisi Watu na tunakoenda inaweza kufika hatua ikawa inatengeneza Maudhui yake yenyewe
Unapotengeneza maudhui kwa AI mfano video au picha ni vizuri ukasema kwani kuna ulazima wa kuwa na Uwazi wa vyanzo vya taarifa tunazozipeleka kwa Umma
AI nyingi bado zipo kwenye experiment stage, kama siyo mjuzi inaweza ikakuletea matatizo
Mwakilishi kutoka Mwananchi (MCL)
Kwetu MCL, AI si jambo la kesho bali ni jambo tunalolitumia. AI imetusaidia katika utendaji kazi, baada ya kutumia siku nzima inaturahishia kwa dakika chache kuzalisha maudhui. Tunatumia zana kama ChatGPT na zana nyingine kuzalisha maudhui ambayo tunapeleka kwa wateja wetu. AI imetusaidia sana katika kuhakiki taarifa, imetusaidia kuzalisha habari za hali ya juu zaidi.
Session - Empowering Tanzanian Content Creators: Monetisation, Ethical Storytelling and Boosting Livelihoods
Maxence Melo (JamiiAfrica): Hii session tunataka kubadilisha jinsi watu wanavyochukulia maudhui ya mtandao. Hatukuwahi kupata nafasi kwa local digital content creators kuwa kwenye maadhimisho ya Uhuru wa vyombo vya habari.
Wazalisha maudhui wengi wa mtandao wapo chini ya umri wa miaka 35, wengi mnapopata nafasi onesheni nguvu mliyonayo. Mpaka umefika hapa, JamiiAfrica imekuthamini sana.
Kwa mujibu wa takwimu za TCRA, wanaotumia intaneti wapo zaidi ya milioni 40. Ulaji wa maudhui upo kwenye dijitali zaidi kuliko kwingine, ila wanaozalisha maudhui yenye tija (Meaningful content) mtandaoni wapo wachache sana.
Nimeongea na META, vikao vingine vya kujengeana uwezo tutakuwa tunavifanya kidijitali ili kuwafikia watu wengi.
Tumia tools tulizozijenga JamiiForums kushirikia mijadala, tupo kama shield kuhakikisha kuwa tunakulinda, hata kule TCRA usiende peke yako. Ili twende pamoja, lazima tushirikiane.
Ukimuona mtendaji wa JamiiAfrica, mfuate akusaidie. Tutaendelea kutoa tools kadri mnavyozihitaji ili muendelee kufanya kazi zenu vizuri.
Sarah Muyonga - META
- Mpaka sasa tuna zaidi ya watu milioni 4 wanaozalisha maudhui Facebook ambao wamepata kipato kupitia maudhui wanayozalisha. Mwaka jana Tanzania ilikuwa kati nchi chache ambazo Facebook reels ilizinduliwa.
Kuhusu ofisi kuanzisha Tanzania, kwa Afrika tuna ofisi Nigeria na Afrika Kusini tu, mimi natoka Kenya ila pale hatuna ofisi, nafanyia kazi nyumbani mara nyingi, ila huwa natoka kukutana na wadau.
Kusaga Tv; Mimi natumia Tiktok lakini naona kama masharti yao magumu maana yanakutaka kwenda live na uwaambie watu watap tap ili uweze kutengeneza kipato. Viewers wengi, likes nyingi lakini hakuna malipo.
Gadi Tv - Nafurahi nimemuona mwakilishi kutoka Meta, nimekuwa nikisikia kuwa watu wanalipwa, naamini leo tutapata madini ya kutosha.
Jeff Msangi- Mwanablogu; Maxence Melo na JamiiAfrica niwashukuru kwa kuwa na consistency, wengine tulikuwep lakini sasa tumepotea ndio maana majina yetu yamepotea. Kuna tofauti kati ya content creators wa zamani na wa sasa, wa sasa mna fursa zaidi sababu mmerahishiwa sana. Urahisi haumaanishi uholela, jitahidi sana kuhudhuria mafunzo yanayotolewa na JamiiAfrica na Meta na wengine ili kuongeza ujuzi.
Katika utengezaji wa content, tengenezeni zinazoakisi mazingira yanayowazunguka, nimeona wengi mnafanya content za kuiga kutoka nje. Content za mazingira ya ndani ndizo zizazoweza kuwavuta meta kuangalia algorithm ya content zinazozalishwa kwa muktadha huo.
Nimeona mmeomba ofisi za meta kuja Tanzania, tengenezeni content za mazingira yanayowazunguka, inaweza kuwavutia META kuja hapa. Tumieni advantage mliyonayo, msilale, mtalala uzeeni. Shirikianeni, msiwe wachoyo, ukiona fursa kama mafunzo ya JamiiAfrica shirikisha wenzako.
Endeleeni kuangalia mbele kwani kwani teknolojia yenu inakwenda kwa kasi, wale mnaoweza rudini shule mkaongeze elimu. Nimegundua AI haikufanyi kuwa mjuzi bali inakuongezea uelewa.
