Uchaguzi 2020 Siku ya 1: WanaCCM 80 wachukua fomu kuwania Ubunge Jimbo la Kawe huku 31 wakichukua Kinondoni

Uchaguzi 2020 Siku ya 1: WanaCCM 80 wachukua fomu kuwania Ubunge Jimbo la Kawe huku 31 wakichukua Kinondoni

Influenza

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2018
Posts
1,509
Reaction score
3,756

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimesema kwa siku ya leo, ikiwa ndio siku ya kwanza ya kuchukua fomu, watu 31 wamechukua fomu kwa Jimbo la Kinondoni huku 80 wakichukua kwa Jimbo la Kawe

Kwa upande wa Kinondoni, mtu mmoja tayari amerudisha fomu na kwa Jimbo la Kawe, watu wanne wamerudisha fomu hizo za kuwania kuteuliwa Ubunge kupitia CCM

Zoezi la kuchukua na kurudisha fomu za kuomba kuteuliwa kupeperusha bendera ya chama hicho katika Majimbo limeanza leo na litakamilika Julai 17 saa 10 jioni
 
Leo ikiwa ni siku ya kwanza kuchukua fomu ya kuomba ridhaa ndani ya Chama Cha Mapinduzi. zaidi ya wanachama 80 wamejitokeza kuchukua fomu katika jimbo la Kawe..

Je ni democrasia?
Jobless?
Kufukuzia uteuzi wa UDC, UDED au UDAS?
au ni wito wa kuwatumikia wananchi umetanuka?
 
Majibu yote ni sawa kulingana na mrengo!
 
Nadhani wote hao wana shauku na nia ya kuwatumikia wananchi wa kawe.

Let's meet at the top, cheers 🥂
 
Leo ikiwa ni siku ya kwanza kuchukua fomu ya kuomba ridhaa ndani ya Chama Cha Mapinduzi. zaidi ya wanachama 80 wamejitokeza kuchukua fomu katika jimbo la Kawe..

Je ni democrasia?
Jobless?
Kufukuzia uteuzi wa UDC, UDED au UDAS?
au ni wito wa kuwatumikia wananchi umetanuka?
Njaa tu
 
Aiseeee. Siku ya kwanza tu 80? Kweli kuna kazi hiyo kura ya kuteua 3 kwa ajili ya kura ya maoni. Dada Mdee itika Abeeeee
 
Mkoa wa Mara siku ya Kwanza tu wamejitokeza 203.

Kituko ni Jimbo la Butiama ambapo mtu na kakake -Madaraka Nyerere na Makongoro Nyerere ni kati ya wagombea 19 waliojitokeza kuchukua fomu
 
Hapo ndo unaweza tuelewa tunaosemaga "Watanzania Ni Wanafiki"

Ok anyway Ni haki Yao kikatiba Ila njaa Ni Mbaya Sana.
 
Hii ni nzuri. Miaka mitano hii ni wao tu walikuwa na airtime. Na wameonesha huko kuna fursa ya kula kiurahisi. Na kwa sababu sheria ya dunia ni survival for the fittest sasa ngoja tupambane huko huko tuone. Huu ndo utakuwa mwisho wa kuchaguliwa na kupotea. Hii ndo mchimba kaburi huingia mwenyewe.
 
Back
Top Bottom