Influenza
JF-Expert Member
- Jul 1, 2018
- 1,509
- 3,756
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimesema kwa siku ya leo, ikiwa ndio siku ya kwanza ya kuchukua fomu, watu 31 wamechukua fomu kwa Jimbo la Kinondoni huku 80 wakichukua kwa Jimbo la Kawe
Kwa upande wa Kinondoni, mtu mmoja tayari amerudisha fomu na kwa Jimbo la Kawe, watu wanne wamerudisha fomu hizo za kuwania kuteuliwa Ubunge kupitia CCM
Zoezi la kuchukua na kurudisha fomu za kuomba kuteuliwa kupeperusha bendera ya chama hicho katika Majimbo limeanza leo na litakamilika Julai 17 saa 10 jioni