Uchaguzi 2020 Siku ya 1: WanaCCM 80 wachukua fomu kuwania Ubunge Jimbo la Kawe huku 31 wakichukua Kinondoni

Sitting allowance ya wabunge wakiwemo mjengoni ya Tsh laki nne kwa siku kila mtu anaitamani ukijumlisha na marupurupu kibao. Godbless Lema alisema kwa mwezi kila mbunge take home pay yake kwa mwezi si chini ya TSh 14 million. Na baada ya miaka mitano unapata kiinua mgongo kisichopungua million mia tatu!

Siku ikitokea posho hizo na kiinua mgongo hicho kikatumbuliwa mambo hayatakuwa kihivi!
 
Awamu hii majimbo ya upinzani ndio hotcake, lazma watu wajazane huko wakiamini kupitia ticket ya "Mboga mboga" ulaji ni wa uhakika.🤣🤣🤣

Na mkulungwa alishagongelea nyundo kuwa wale ma MP wa mrengo wa kushoto wajiandae kuambulia asante kwa kushiriki! Round hii mjengoni watapasikia kwenye vyombo vya habari tu.😂😂😂
 
Ndugai achukue form kwanza nyumbani kwake kabla ya kwenda kwenye tawi la chama. Ajipime Kwanza kama anakubalika kwenye kura za maoni ya familia.
 
Ubunge ndio biashara inayolipa zaidi kuliko zote, Ingekuwa ni kazi ya kujitolea tungepata wawakilishi wa kweli wa wananchi.
Unalala tu bungeni na pesa zinaingia tu,ukimaliza tu ubunge pesa nyingi unalipwa kuliko hata injinia au daktari aliyefanya kazi miaka 40
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…