Siku ya kwanza baada ya kufungua kibanda umiza

Shukrani san mzee naamini ni swala la mda tu
 
Kwa uzoefu wangu wa kibanda umiza mwaka wa pili sasa, nilichogundua kuna soko tofauti kwa michezo tofauti, mfano kuna mtu ambaye ni mshabiki wa timu kama simba na yanga hivyo huwezi kumkosa kibandani zikicheza timu zake, kuna wengine ni machizi wa mpira wa bongo yani yeye hata icheze gwambina na mwadui lazima aje ila watu hawa sio wengi sana, kuna wengine wanapenda mipira ya ulaya ila wanaangalia timu zao tu na kuna kundi lingine wanaangaliza mechi zote iwe ulaya au bongo, hiyo michezo uliyotaja ina mashabiki wake ila kiasi cha biashara utayoiyanya hailingani na kuonesha mpira ukichangia michezo mingi ipo weekends, kibanda umiza unauza huduma hivyo inategemea na jamii inayokuzunguka, kuna mitaa wanaonesha hadi nba inayopigwa saa 11 alfajiri kwasababu soko lao linaruhusu, ushauri wangu aanze taratibu baada ya miezi miwili atapata wale watazamaji wasiopenda kelele mabanda mengine, ni muhimu sana kujua kwann wanakuja kuangalia kwako, mm niko uswahilini kabisa wateja wangu nimewateka kwa huduma zingine tofauti ya mpira wanaoufuata.
 
Acha roho mbaya mkuu!
 
dstv ni pasua kichwa achana nao tafuta mbinu nyingine ya kuonyesha ligi za ulaya kwa gharama nafuu
 
Ushauri games zote za bongo onyesha bureeeee... maana ndo vibanda umiza vingi vinafanya...
 
Mkuu kwanza hongera kwa kujaribu ila jua biashara ina chanagamoto sana ikiwa changa cha msingi kama unaona watu hawavutiki jitahidi uweke na vinywaji hapo kisha weka bure kuangalia hata gemu mbili ili pafahamike yote hayo yaambatane na uboreshaji wa huduma.
 
Hii kweli kule mbagara rang tatu kuna ukumbi unaitwa emirates ni wa kawaida tu lakini watu huenda pale kwa sababu ya ubishi kuna jamaa anaitwa Salum mshabiki wa Arsenal na Nando mahabiki wa Liverpool hawa watu mwenye ukumbi hawadai hela hasa huyo Salum maana ndo wanaleta amsha amsha sana wakiwepo hao ukumbi wote unakua kelele mwanzo mwisho....

Yule mmiliki wa huo ukumbi kwa sasa ana duka kubwa sana la jumla la kuuza bidhaa mbalimbali za vyakula na pia ana Costa kama sikosei 2 kwa biasharahiyo.
 
KUNA SEHEMU NILIKUTA VIJANA WA CHUO WAMENUNUA SMART TV KWAAJILI YA KUONESHA MPIRA KWENYE KIBANDA UMIZA.
ILI KUEPUKA GHARAMA ZA DSTV WAO WANACHOKIFANYA NI KUTAFUTA CHANEL INAYOONYESHA MPIRA MTANDAONI KUPITIA SIMU KISHA WANAWASHA BLUETOOTH YA SIMU NA TV HIVYO MPIRA UNAONEKANA VIZURI TU KWENYE TV.
HAPO HATA MVUA IKINYESHA ZILE KERO ZA DISH KUSCRATCH HAZIPO LABDA MTANDAO TU ULETE SHIDA.
 
Nakupongeza kwa kuthubutu, cha msingi ni uvumilivu baadae mambo yatakuwa sawa tu
 
Hii teknik Ni nzuri
 
Shida ya Bongo network mkuu
Binafsi huu mwaka wa 2 sijaingia kibanda umiza huwa naangalia mechi kupitia simu ila siku zingineNetwork changamoto
 
Tupe mrejesho baada ya leo kutoa offer, mechi ya simba ..
 
πŸ˜πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
Sio kwamba nakucheka lkn mkuu
Mi sikuchek
 
Kuna channel za muvi kali,Kuna channel za wwe za mieleka ya akina roman reign.je ukjiongeza hapo kuna tatizo.?
Au hivo vibanda ni kwa ajili ya Mpira tu?
Yupo kijiji? Je watu wa kijiji wanajua kuhusu WWE?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…