Siku ya kwanza baada ya kufungua kibanda umiza

Tatizo network huku mwisho kabisa 3G
 
Leo nimetoa ofa kama wadau mlivyonitonya ambapo kimsingi walikuja watu 21 nikatumia nafasi kuwaambia jmosi ni jero jero na saivi niko na wana hapa kama kumi tunacheki uefa free
Kaza buti mkuu siku zote uvumilivu Ni kitu mhim Sana,kwa hiyo wewe amini tu kadiri siku zinavyoenda na ndio mambo yatazidi kuwa mazuri na ujitahidi kuboresha mazingira...
 
Hauna mkono wa biashara!!!

Hili neno naomba ufafanyzi mkuu.
 
Komaa mwanzo mzuri kwa baadae weka na spika moja nje iwe inapiga sauti hua inaleta mzuka pia utaongeza na screen ukubwa angalau uwe na moja ya inch 49
 
Mleta mada umeanza vizuri biashara yako cha msingi ni kukomaa ili watu wapazoee mimi nilianza hii biashara mwaka 2013 maeneo ya Chanika pasipokuwa na umeme nilikuwa natumia Generator now mimi ndo top kama leo mechi ya Simba vs Kagera Sugar nimefunga na kiasi cha 48,000= bado Uefa cha msingi ni kukomaa
 
Watu wanapenda sana ukumbi uwe na amsha amsha pamoja na mashabiki wabishii
 
Nataka nitumie jmos kama kipimo hio game y watani wa jadi
 
Unapanda mbegu Leo unataka uvune kesho?!! Biashara inaanza kupimwa ndani ya miezi 3 na kuendelea.

Biashara isiyo na hasara ni UTAPELI pekee
 
Shida ni kwamba sisi wa afrika tunaanzisha biashara na mtaji kiduchu sana,ndo maana tunakuwa tunafeli mapema sana,tujifunze kwa wenzetu wa asia ambao wao wameonyesha mafanikio makubwa ktk ujasiriamali,kwa kipindi hiki kifupi ulichoanzisha biashara hukupaswa kufikiria mambo ya vifurushi n.k ..usikute na kula napo unategemea hapohapo ..biashara ni kama mtoto unapaswa uilee hata kwa mwaka ndo ufunge mahesabu,la sivyo itakupa sana mawazo,itakuendesha badala ya wewe kuiendesha yenyewe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…