Siku ya kwanza baada ya kufungua kibanda umiza

Siku ya kwanza baada ya kufungua kibanda umiza

Ni takribani siku moja sasa toka nifungue kibanda umiza maeneo ya hapa kijijini japo sio kijijini sana ambacho nilikipa jina la "VPN ARENA"

Nimeweka both dstv na azam bila kuchelewa nikarusha matangazo ya game ya jana ya yanga na biashara nakufanikiwa kupata wateja wanne(4) tu kwa kiasi cha jero jero.

Kwa wazoefu naombeni mawazo yenu kua kweli nitapata japo hela yakulipia kifurushi cha dstv ambacho ni 89000 compact plus na azam mwisho wa mwezi? [emoji848][emoji848][emoji848]
Njoo inbox mzee 0712043374 tupeane uzoefu
 
Kuwe na hewa safi watu wanakwapa plus mdomo kunuka duh
 
Pia jitahidi kuwafahamu mashabiki wa timu kubwa wenye ubishi na maneno nengi na kuwaweka karibu ikiwezekana kuwapa ofa ya kutazama game bure hapo kwako itakuongezea wateja wengi sana watu wengi huwa wanapenda majibizano wakati mechi zinaendelea na baada ya mechi kuisha.
Umenichekesha sana ulivyotaja watu wabishi na maneno mengi,hao kila mtaa huwa hawakosekani[emoji38][emoji38][emoji38][emoji38]
 
Hakuna mpinzani ni mimi tu!!
Simba na yanga niweke jero au buku mkuu!!
Jero, ukitaka ku penetrate soko,, shusha bei, ongeza thamani,,
Mfano weka kijiwe cha kahawa upenuni, weka banda uuze sigara, pombe za kupima, etc
 
Back
Top Bottom