Siku ya kwanza kuamkia kwenye nyumba yako, furaha yake usipime!

Hongera sana ndugu yangu. Ni kweli... kipya kinyemi. Unaweza kunenepa ghafla just kwa kuangalia nyumba yako tu. Na kama ulivyosema siku ya kwanza ukiamka asubuhi unakuwa umejawa na furaha kubwa sana. Enjoy your new home man!
 
Kama gharama za usafr Ni sawa na gharama za kupanga Ni Bora tuendelee kupanga

Nilikuwa na akili kama zako mpaka pale nyumba niliyopanga ilipouzwa bila mimi kupewa taarifa na nikiwa bado na mkataba!! aliyenunua akaja na vyombo vyake anataka kuingia ndani .. kesi zikaanza na amani ikatoweka ..muda wa kwenda kazini we unaenda kumsubiri mwenyekiti wa serikali za mtaa kusikiliza shauri lenu.. mwenyekiti naye keshapewa cha juu anakuambia bora utafute nyumba nyingine.. ukirudi home wife anakuuliza vipi mmefikia wapi.. ukitazama dogo anacheza na wenzake nje kwa furaha hajui kama pale sio kwao tena!!.. acha kabisa!..
 
Hongera sana ndugu yangu. Ni kweli... kipya kinyemi. Unaweza kunenepa ghafla just kwa kuangalia nyumba yako tu. Na kama ulivyosema siku ya kwanza ukiamka asubuhi unakuwa umejawa na furaha kubwa sana. Enjoy your new home man!
Hahahaha!!!

Kingine ile harufu mpya mpya ya nyumba inayonukia. Kingine ile nyumba mpya na vitu vipya ndani ya nyumba.

Halafu ukimuangalia mkeo na watoto jinsi walivyo na furaha. Ni kweli ulichokinadi, unanenepa kabisa.
 
Kujenga wanajenga Strabag na Estim...wewe umepanga matofali umepata hivyo vyumba vyako vi3 unakuja kutishia watu humu
 
Unataka kutuambia malipo yako pale Lumumba buku Saba yamefanikisha kutoa kamjengo?

Polepole basi aliwapa kipaumbele kipindi hiki cha anguko lenu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…