Siku ya kwanza kuamkia kwenye nyumba yako, furaha yake usipime!

Siku ya kwanza kuamkia kwenye nyumba yako, furaha yake usipime!

Furaha ya nyumba mke....kuna watu wameamia Kwenye majumba yao lakini baada ya siku kadhaa wamezkimbia nyumba zao wamerudi kupanga tuu...kisa gubu la mke

Hongera mkuu kama mke nae yupo vzuri furaha yake inaongezeka mara dufu
 
Nilikuwa na akili kama zako mpaka pale nyumba niliyopanga ilipouzwa bila mimi kupewa taarifa na nikiwa bado na mkataba!! aliyenunua akaja na vyombo vyake anataka kuingia ndami .. kesi zikaanza na amani ikatoweka ..muda wa kwenda kazini we unaenda kumsubiri mwenyekiti wa serikali za mtaa kusikiliza shauri lenu.. mwenyekiti nae keshapewa cha juu anakuambia bora utafute nyumba nyingine.. ukirudi home wife anakuuliza vipi mmefikia wapi.. ukitazama dogo anacheza na wenzake nje kwa furaha hajui kama pale sio kwao tena!!.. acha kabisa!..
Pole sana Mkuu. Kisa chako kinasikitisha ingawa hujakielezea vizuri.
 
Hahahaha!!!

Kingine ile harufu mpya mpya ya nyumba inayonukia. Kingine ile nyumba mpya na vitu vipya ndani ya nyumba.

Halafu ukimuangalia mkeo na watoto jinsi walivyo na furaha. Ni kweli ulichokinadi, unanenepa kabisa.
Ile harufu huwa inaishaga na kujamba.
 
Hongera zako Mkuu. Ni stage kubwa mno hiyo na unapoifanikisha kwa hatua yeyote ile huna budi kumshukuru aliye juu.

Kwani si wote wanafanikiwa kuufikia uhalisia walio wengi wanajenga maghorofa na nyumba mawazoni tu.

Ziwafikie kwa kweli.
Ila kipindi cha mvua baba wenye gari ndio uwa juu mawinguni 😀
 
Back
Top Bottom