Hakuna kitu kinaumiza kama kuishi kwa ndugu, naamini ipo siku nami nitakuwa na kwangu.
Sikupingi ndg lakini tuna vitu pia sisi tunashindwa kwenda navyo tunapokuwa kwenye nyumba za watu,,watu kutaka kuishi kama waonavyo wao na si kama mwenye nyumba atakavyo au taratibu zake zilivyo,,wengi wetu tunataka tujiendeshe kama vile uko kwako! Hapana!
Wengi wetu hata vikazi vidogo tu vya nyumbani hatutaki kufanya,,na hatuwezi kuchukuliana na mazingira mapya.. Mim nililelewa na baba mdogo na mama mdogo (RIP Mama), niliwakuta wakiwa na bint wa Kazi tu na nikaendelea kuishi hapo tangu mdogo,,mama alikuwa very straight na nilijitaidi kushi vizuri.
Alikuja bro mmoja alishindwa kwa sababu ambazo mim naziona ni ujinga tu,,Kazi za walezi wetu waliokuwa wanalazimika kurudi jioni Sana,,sasa jamaa yeye hata akiwa yupo home hawezi fanya chochote jikoni anamsubiri mama maana Kuna kipindi mfanya Kazi aliondoka...hii mama mlezi hakuivumilia kbs..jamaa nae anapanda juu kwamba yeye mwanaume hawezi pika n.k mwisho aliondoka...
Majuzi Nina mdgo wangu kbs upande wa mke wangu,,Mungu wa rehema ametusaidia tuko kwetu,,sasa jamaa hataki kuchota maji na eneo niliko maji hayajafika,,yaani mtu ananuna Sana akipewa Kazi kusaidia,,
Hitimisho langu sisi tunakoaa kwa watu tujitaidi kwenda na mazingira ya nyumba husika,,wachache wenye kuonea...let's be smart.