Siku ya kwanza kuamkia kwenye nyumba yako, furaha yake usipime!

Miaka mi5 ulikuwa unajenga Ghorofa? Kama nyumba zetu hizi ramani kidole ni ndani ya miezi 6 tu ushamaliza!
 
Wakuu, ninakuja kwenu kijana ninayetaka kumiliki mjengo!

Nina mil 8! Kiwanja ninacho chanika! Kipo tambarare ardhi ni Mchanga.

Mchanga roli la 15m3, ni 250,000, maji yapo karibu Ni kufunga tape tu.

Nyumba ya sebule, master, jiko, store.. njoo Cha ndani Cha kawaida.

Kwa pesa hiyo naweza kujenga Boma, kuezeka, plaster, na kufunika paa pamoja na milango na madirisha ya grill?
 
Wakuu, ninakuja kwenu kijana ninayetaka kumiliki mjengo!
Nina mil 8! Kiwanja ninacho chanika! Kipo tambarare ardhi ni Mchanga...
Hapana utalipua... kama huna dharura sana jenga taratibu nyumba yako ...finishing ya nyumba ni gharama ..nenda taratibu utakapoishia pumzika, vuta pumzi then endelea utapata nyumba nzuri sana
 
Umaskini ni pale kijana anapowaza kujenga nyumba badala ya biashara
Akili zetu zina shida kubwa sio kidogo
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] Dah pole sana hiyo stress yake sio ya kitoto bora ukaishi kwenye nyumba yako ambayo haija Isha kuliko fedheha kama hiyo
 
Umeongea kwa hisia na nimekuelewa sana mkuu. Ukweli lazima usemwe, nyumba ya kupanga huwezi kuwa na amani, ni kheri gharama kubwa ya usafiri lkn nipo kwangu
 
Fact kabisa hii. Unapoishi endana na mazingira ya mahali husika. Kipimo cha utu ni kazi, ikiwa mtu hataki kazi basi huyo hana utu, hafai kuishi naye
 
Hiyo ni shida! Kufuliwa chupi graduate?
 
Umaskini ni pale kijana anapowaza kujenga nyumba badala ya biashara
Akili zetu zina shida kubwa sio kidogo
Nilidumbukiza 30M kwenye biashara, biashara imekufa within 3 years, na nyumba sina. Heri hiyo pesa ningeanza kujenga nyumba sasa hivi ningekuwa na mahala pangu pa kujisitiri ndio nianze kuhangaika na biashara.
 
Umaskini ni pale kijana anapowaza kujenga nyumba badala ya biashara
Akili zetu zina shida kubwa sio kidogo

Biashara sio kwa kila mtu! Mwingine hiyo pesa ataipeperusha asubuhi kabla jogoo hajawika.
Mtu anaweza kujenga nyumba yenye thamani kubwa lakini sio kwamba alikua na hiyo pesa yote kwa mara moja.
Kwa mfano huyu jamaa kajenga kwa miaka mitano, unaweza kukuta alianza kujenga akiwa na milioni moja au mbili.
Akajichanga kidogo kidogo tena akaendeleza hadi kuja kukamilisha. Usimlaumu sana ila wewe unaweza kuweka ushuhuda wako hapa kama ambavyo yeye ametuletea wake wa maamuzi ya kujenga.

kitu nakubaliana nawewe ni kwamba wengi wetu hatuna elimu ya uwekezaji/ Biashara.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…