siku ya kwanza nimefika shule kesho yake ikawa shamba(nilihamia kutoka day nikapelekwa bording) nimefika shamba nimepangiwa mistari nane ya mahindi ya kupalilia tangu nizaliwe sijawai kulima nililia hatari akaja dada mmoja wa mwanza akaniambia atanisaidia kulima alilima fasta kufumba na kufumbua amemaliza nikamnunulia mkate akanywa na chai enzi zile mikate ya skoz,mpaka namaliza pale sikuwai kulima wala kupalilia mimi naenda shamba kupiga story natafuta wale wa kijijini nampa mkate analima kipande changu chote.
dada angu aliyenilea alikua anafanya kazi supermarket tranka langu lilika na vilonzo hatari mambo matamumatamu na kila mwisho wa mwezi anakuja kunitembelea.
kuku ,bata wa walimu tushaiba sana tu usiku tunaenda jikoni tunachemsha tunakunywa supu na nyama tulikua watundu sana ,kuna siku sasa tuliiba mbuzi wa mwalimu dhaaa sitasahau tulimchinja wenyewe,chuna wenyewe,tulikula usiku kucha ile siku,daaah shule ilikua raha sana nilikua kibonge nilirudi nyumbani mwembamba ugali ,uji ,vilinishinda kabisa nikawa nashindia mkate na juice.
changamoto za maisha natamani nirudi vile,nilikua sina stress yyt ile ninachowaza nikadibue maji ya nani nikaoge ,maisha yalikua mazuri siwazi yyt yule sina anayenitegemea daaah,sahizi nikiwaza ada ya shule january natamani nigeuke malaika nipae mbali na majukumu .