Siku ya kwanza kuingia shule ya bweni ya Serikali

Siku ya kwanza kuingia shule ya bweni ya Serikali

Nashukuru kwa hizi experience zenu,natarajia kureport form5 muda si mrefu......
 
Ambao hatukusoma tutaambia Nini watu??[emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24]
 
Mimi nakumbuka ilikuwa shule ya Sokondari Bagamoyo enzi hizo ilikuwa ni day and boarding school. Wasichana na baadhi ya wavulana wachache sana walikuwa day walikuwa hawafiki hata mia kwa ujumla wao nikakuta vijana wanaita Bagamoyo Boys High School wakati kuna wadada, nilipo fuatilia sababu nikaambiwa wale wadada walikuwa na sura kama za wavulana. Isingekuwa sketi zile zenye rangi nyekundu mtu angedhani wote ni boys kweli!
Kwa jina lengine miembe saba?
 
Nililia kama vile nimeachwa peke yangu kaburini, ilipofika jioni daah nikazidi kuvurugwa, akili ikanituma kesho nikiamka tu nitatoroka nirudi nyumbani,..... Ila nilikuja kuzoea nikachukulia kawaida, makande sikuwahi kula huko nyuma, ila pale niliyakuta na kuyapenda kuliko wali....
 
kitendo cha kusimama kwenye foleni ya chakula na sahani mkononi kilinichukua muda sana kukizoea

nilijua muda wa kula kuna meza labda kama nyumbani,ila muda wa kula kengele nkaskia mara naona kila mtu na sahani

namimi nkashka sahani nkajua tunapeleka mezani kumbe n folen,baada ya kupewa msosi najua labda kuna ssehem ya kwenda kula

eti kumbe unatafuta unapopajua wewe unakula msosi wako ukmaliza kaoshe sahan yako kahfadhi kwa tranka,asee week ya 1 kila kitu kwangu kilikua kama nipo adventure.
 
Back
Top Bottom