Form 5 nilipangiwa na shosti angu tena comb moja..... Tukaenda wote tumevuuta hatari tumefika shule tunajikuta masista duu wajanja ndo sis asubuhi tunashangaa kuamka saa kumi na moja asubuhi hapo unapangiwa kufagia uwanja mkubwaa,afu umwagilie garden mpaka iwe tifu tifu baada ya hapo ukadeki choo afu saa moja sharp uwe parade ....aisee ikabid niulize hiz Kazi mpaka lini nikajibiwa ndo maisha ya kila siku niliangua kilio kisicho na mfano siku ya kwanza nikasema haya maisha siwez ,
Mda wa parade nipo na shati la tomato kidogo dogo na sketi ya kisista duu ya kiunoni nilikua nmeshashona home mwee mweee mwalimu kupita akatutoa mbele kwamba m shoga angu tumevaa kihuni tukapelekwa kwa Fundi wa shule tukashonewa mpaka shati kubwa kama la baba paroko kitamba kama cha shuka daa huku sket ya tumboni ndefu hatari
Nilienda na kikombe cha udongo kidogo dogo cheupe kama cha kahawa vile na kisahani changu kidogo kama kisosi maana o'level shule niliotoka full ubishoo ,doooh kufika SAA nne uji madai hatunywi tumbo litakua kubwa afu nashangaa watu wana majagi hahahaha..... Mwezi mrefu nikatafuta jagi langu na bakuli kubwa tu tena la plastic uji nikaunywa vizuri tuuuu na foleni ya ugali nikapanga
Shule ilikuwa kanda ya ziwa washamba washamba wengi tukaanza kuwacheka wahaya kwamba mjini wanajishauaga saana ila kumbe wana lafudhi mbovu inshort ni wakuja tuu tuliwacheka saana....
Nakumbuka siku ya kwanza tu nilipiga simu nyumban maisha magum siwez mzee akanimbia vumilia mpaka muhula uishe ndo utahama ,sasa muhula daah Kazi nying afu viongoz walikua wanaishi kwa raha saana hawafanyi kazi yeyote nikaona bora nikimbilie uongoz bahati mbaya viongoz wote form6 na uchaguz mpaka muhula wa pili ,siku ya kufunga niliondoka na kila kitu changu kufika nyumban shule nilizotaka kuhamia background ya result zao kwa comb yangu sio nzur tena wasichana ndo kabisa div3 , div4 na 0 maana nilikua pcm nikasema hapana bora nilipotoka comb yangu wanafaulu nikarudi baada ya miez miwili na tranka langu hahahaha nikakuta mwalimu wa zamu mnoko hatari akanipa adhabu ya kuvuta akanikatia shamba la kulima na kuchimba na kuzisombelea molam ndoo 25 ,shamba nikaajiri wanakijiji kimbembe molam anasimami nikabeba kufika ndoo ya 10 viungo vya mwili vikagoma havina ushirikiano kabisa naumwa kila sehemu nalia hatari nikarud Dom nikampigia mzee nikamwambia akasema nipe namba za mwalimu wako nikampa sijui waliongea nin baadae nashangaa naitwa sikwenda mwl akaja nipo kama nakaribia kufa akaniambia adhabu umesamehewa
Muhula wa pili baada ya mda ikafika kipind cha uchaguz nikasema hapa lazima niwe kiongoz kwa mikaz ya shule naweza kufeli bure nikachukua fomu bahati nzur kichwani nilikua vizuri nikachaguliwa academic
Baada ya kuwa kiongoz ndo maisha yakaanza sasa kwanza nikachagua room nayotaka ,ambazo nitofaut na wanafunz wa kawaida ndani mnakaa wawil tu chumba mapazia ,carpet hapo ndo nikaish kama nipo chuo mpaka namaliza .....
Nashukuru tu Mungu nilifaulu vzuri