Siku ya kwanza kuingia shule ya bweni ya Serikali

kwayu headmaster wangu azaboy namkumbuka sana huyu mzee alikua kama baba mzazi shuleni
 
[emoji13][emoji13][emoji13][emoji13][emoji13]watu mna matukio aisee
 
Vyema
 
Hahahahahaha
 
December 1.

Nataka nianze maandalizi ila kuanzia kesho kutwa ikiwezekana naenda Makao makuu nikajiandikishe mkataba wa Practise wizarani
Mwambie la profeseri akusaidie. Tafuta na kiwanja haraka. Mwambie G. akutafutie.
 
siku ya kwanza nimefika shule kesho yake ikawa shamba(nilihamia kutoka day nikapelekwa bording) nimefika shamba nimepangiwa mistari nane ya mahindi ya kupalilia tangu nizaliwe sijawai kulima nililia hatari akaja dada mmoja wa mwanza akaniambia atanisaidia kulima alilima fasta kufumba na kufumbua amemaliza nikamnunulia mkate akanywa na chai enzi zile mikate ya skoz,mpaka namaliza pale sikuwai kulima wala kupalilia mimi naenda shamba kupiga story natafuta wale wa kijijini nampa mkate analima kipande changu chote.

dada angu aliyenilea alikua anafanya kazi supermarket tranka langu lilika na vilonzo hatari mambo matamumatamu na kila mwisho wa mwezi anakuja kunitembelea.

kuku ,bata wa walimu tushaiba sana tu usiku tunaenda jikoni tunachemsha tunakunywa supu na nyama tulikua watundu sana ,kuna siku sasa tuliiba mbuzi wa mwalimu dhaaa sitasahau tulimchinja wenyewe,chuna wenyewe,tulikula usiku kucha ile siku,daaah shule ilikua raha sana nilikua kibonge nilirudi nyumbani mwembamba ugali ,uji ,vilinishinda kabisa nikawa nashindia mkate na juice.

changamoto za maisha natamani nirudi vile,nilikua sina stress yyt ile ninachowaza nikadibue maji ya nani nikaoge ,maisha yalikua mazuri siwazi yyt yule sina anayenitegemea daaah,sahizi nikiwaza ada ya shule january natamani nigeuke malaika nipae mbali na majukumu .
 
Walala mnaiba mbuziii???[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
 
Mkuu kitemango kipindi hicho alikua ameshondoka mkuu , mwaka 2006 mkuu alikuepo Andrew kwayu , kwayu alikua POA Sana mkuu

oooh, 2006 nillikuwa nishatoka. Kumbe neema ilikuja baadae.
 
Vipi huyo Mbuzi mliyemuiba hamkushtukiwa?
 
Kilicho nikelaga shule za bweni ni kunguni tu baridi lilichangia Sana watu kua wachafu na kupelekea watu kua na mifugo mingi ( kunguni ) usiku ulali vizuri kabisa , mbeya moja iyo mbalizi sec
Hii siyo ya serikali, kafungueni Uzi wenu na wenzako mlotafuta nao credit kabla ya kuanza advance... Huu Uzi ni kwa ajil ya watu tuliofaulu na kusoma shule za serikali
 
Hahahahaaaaaa!! Kaka shemeji kama nakuona ulivyolalia chaga.
Acha tuu nilikuwa mjinga flani hivi yani baaada ya kuanza kwenda class wajamaa wa form three wao hawafui mashat kazi yao ni kuchukua kwenye kamba hata kama lina jina lako. Halafu wanarudisha likiwa chafu....

Ukifua nguo lazima ukae mita kadhaa pale uzilinde zikauke zisiibiwe. Yan kama vile ule mwaka 2o15 watu walivyokuwa wanalinda kura

Baada ya kujanjaruka sasa dada shemeji.....
 
Hahahaaaaa!! Ukawa mwizi ulokubuhu[emoji85][emoji85]
 
Hayo yote yalitokea siku ya kwanza unaripoti!!!!!!
 
Hahahaaaaa!! Ukawa mwizi ulokubuhu[emoji85][emoji85]
Acha tuu. Kazi kuiba sukari na yale maziwa ya unga. Yaaan sukari ilikuwa bizaa admuu saaana. Ukiwa nayo asubuh uji utakunywa fresh makande utakula fresh. Pia utauza.
Mungu atusamehe kwa kuiba sukari
 
Went to old moshi pia
Meru pia
 
Hahah, I see a brother. Itakua waluguru walizipeleka Mongwe.Nyayo!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…