Pakawa
JF-Expert Member
- Mar 11, 2009
- 7,973
- 13,647
Hahahh mate umenikumbusha mbali sanaIlikuwa form V, baada ya orientation, tunes za kujuana. Wengi tulishapewa majina ya rafiki wa rafiki ambae anakuja shule ile.
Dining siku ya kwanza mdada mmoja akimwaga magarage kisa alimkuta mende ndani ya bakuli. Kwakuwa bado tulikuwa na makula kula kuna waliomtengenezea orange squash na marie biscuits.
Baada ya miezi miwili pale shule, mdada alikuwa hodari wa kutoa mende kwa kijiko na kuendelea na menu.
Baada ya kutoka shule za private kuingia shule za serikali First day was a nightmare
Kuoga ndio ulikuwa mtihani mkubwa kwani watu walikuwa wanajimwaga kama walivyozaliwa kwa kadamnasi hahahhh huu mtihani ulikuwa mgumu kuukamilisha. Tuje kwenye mlo kuanzia breakfast mpaka supper hili lilikuwa zoezi gumu sana maharage daily samaki sato once a week (harufu ya hapo anajua Mungu) chai na mkate nusu una wadudu sijui nyenyele wale ilikuwa balaa (thank God ule uji wa kuongezea chumvi ili sukari ikolee haukuwepo pande hii) Sasa tuje kwa ubwabwa na nyama ya ling'ombe hahahh pilipili hoho tu ndio zilikuwa zinachangamsha mlo.
After few months tukazoea na kuwa hodari wa kununua mihogo na kuunga maharage tena (kujipikilisha)
*** All in all tulijifunza mengi
*** miss maisha ya shule