Siku ya kwanza kuingia shule ya bweni ya Serikali

pole sana mkuu
 
Akina sisi wa Mzizima na Shaaban Robert tunacomment wapi jamani?!
 
Ile Kilamanjato Boys noma sana wenyewe tuliita "Kiliboys" hapa nakumbuka:-
1. Dogo mmoja form one ilikuwa siku ya ijumaa mchana ni makande hapa kunakuwa na vurugu sana bwaloni, yule dogo kawahi kajaza sahani akala kiasi kilichobaki akafungia kwenye mzinga(sanduku la chuma) ili jioni aendelee na makande yake asipange foleni ya ugali, wahuni wakamtaim ametoa wakageuza sanduku lile chini juu na kulitikisa sana kisha wakalirudisha kama lilivyokuwa. Pata picha alivyokuja kufungua sanduku baadae, ikumbukwe sanduku hili ndio lina kila kitu kuanzia uniform na vitu vingine.

2. Uzuri wa hii shule hakuna kukacha prepo ukajificha bwenini, mabweni yalikuwa na vibwengo sana hasa hasa bweni la horombo.

3. Shule ilikuwa mbali sana na wilayani, haina fensi huwezi hata kutoroka ni pori tupu na kuna tembo porini kutokea Kenya.

SIKU HIZI NASIKIA IMEPOA IMEKUWA SHULE YA WANAWAKE.
 
Waafrika tumezaliwa na roho ya ukatili, eeh. Kumbe tusimlaumu Jiwe. Ukatili ni asili yetu.
 
Mwaka 1992 wakati naanza boarding form i ilikuwa balaa sana,mbeya moja hiyo baridi kama lote hata kufua ngumu mikono inauma balaa.
Blanket nilikuwa ninarudisha home enzi zile hata washing machine hakuna. House boy alikuwa anapambana nalo
 
Hubby alisoma hapo alitoka na Div One O level
 
Noah hongera, boarding mimi nilianza Primary lakini shule za RC zilikuwa na tofauti kubwa na za serikali.
Shule za RC kabichi lililaangwa kwa Nyanja na kitunguu na ugali wa sembe kama home tu .
 
Wakati naripoti kidato cha 1, mzee alinipeleka hadi shuleni. Nilipofika shuleni, nikakabidhiwa kwa mwalimu wa nidhamu. Mzee alisoma shule za zamani za mkoloni. Akawa anaongea Kiingereza na mwalimu wa nidhamu lakini mwalimu anajibu kwa Kiswahili. Mzee akaruhusiwa kuondoka. Alipoondoka, mwalimu akanikabidhi kwa kijana mmoja ambaye alikuwa kidato cha 4 anipeleke bwenini. Tulipofika bwenini. Yule bwana akaanza kuongea kimombo huku akiwaambia wenzie, "we have a newcomer". Nilikuwa siwezi kuongea kimombo lakini kwa mbali nilikuwa naelewaelewa. Huyu wa kidato cha 4 alikuwa anasoma na kijana mmoja anayetoka kijijini kwetu. Kwa hiyo akaniunganisha kwake. Maisha yakaanza.

Kulikuwa hakuna maji shuleni. Kula ni mpaka uchote maji mtoni kwa ndoo na kuyapeleka jikoni. Kazi ambayo wanafunzi walifanya kwa zamu. Kuoga lazima uende mtoni. Kwa vile ilikuwa mkoa wa Kagera, kulikuwa na kazi ya kumenya ndizi kwa chakula cha shule. Usipomenya, hakuna kula. Hili nalo tulilifanya kwa zamu. Chooni ukiingia, utanuka harufu ya choo kwa saa nzima baada ya kutoka. Kwa hiyo, kupunguza harufu, unavua nguo na kuziacha nje kabla ya kutumia choo. Juma la kwanza shuleni, niliharisha sana. Nikata kuacha shule. Ila pesa zangu alikuwa nazo yule kijana tunaetoka naye kijiji kimoja. Nilipomuomba pesa ili nirudi kijijini alikataa kunipa. Kidato cha pili walikuwa wanatuvamia usiku tumelala na kutupiga na kukimbia. Kuna wanafunzi wenzetu wawili waliamua kuacha shule na kurudi kijijini kwao! Mateso yalikuwa ni mateso.

Mungu anisamehe. Umasikini unaweza kufanya ufanye mambo mabaya na ujute. Wakati bado niko O-level, kuna siku nilitapeli. Nilikuwa sina pesa. Nikamuuzia mtu tiketi ya meli iliyokwisha tumika. Na mimi pia nilikuwa nasafiri siku hiyo. Ili nisitambulike kirahisi, nikabadilisha nguo baada ya kuuza tiketi. Wakati nakwenda kupanda meli, nikamwona niliyemuuzia amekataliwa kuingia katika meli. Na akaniona na kunitambua japo nilikana. Nilichukuliwa juu juu na kupigwa makofi lakini niliendelea kukana. Mwishoe waliniruhusu kuingia katika meli na nikamwacha yule bwana. Sijui aliruhusiwa kusafiri ama la. Kwa kweli ili jambo bado nalijutia hadi leo.

Nilichofanya ni kuwaepusha watoto wangu na maisha ya aina hii.
 
Siku ya kwanza nafika shule nikamtongoza mama mmoja alikua mpishi Wa canteen ya shule..akanikubali basi nilikula bure canteen mwaka mzima lakini nikaja kutembea na mtoto wake aliekuwa anasoma hapo kidato cha pili hapo ndipo huduma za mama zilipokata ila mtoto akawa ananihudumia zaidi ya mama mtu
 
Duuh...[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]Ukalaa mama na mwana
 
Yaani hapo ni kidato cha 1? Nyie wengine naona mlikuwa tofauti na mimi. Mimi wakati niko kidato cha 5, ndevu zimeanza kutoka sasa, niliwahi kupendwa na msichana aliyekuwa anafanya kazi tayari. Alikuwa anafanya kazi TANESCO wilayani. Basi mchezo mchezo tu aka-fall in love. Akanikaribisha nyumbani kula chakula cha mchana nikaenda na mshikaji. Tukala, akatupa pesa, halafu tukaondoka. Weekend nyingine akanikaribisha pia, nikatokea na mshikaji tena. Tukala halafu tukaondoka. Baada ya muda kupita, akanikaribisha chakula cha jioni. Safari hii akasema niende mwenyewe tu. Hapo ndio nikafunguka macho. Sikwenda na mchezo ukaishia hapo. Mtu aliyetaka kunitoa kwenye mstari wa masomo wakati huo, sikumwelewa kabisa.
 

Krokomu!
Katika shule za kanisa katoliki zilizoshindikana.
 
Aisee...ilikuwa hatari sanaa! Hilo ziwa inaelekea lilikuwa na kina kirefu sana daah...
hatari mkuu ni mazuri kusimuliwa ila huo usiku ulikua ni wa shida sana, shule ina hadi walemavu wa ngozi, wasiona, na viwete lakin hawa jamaa ffu walivyofika skonga hawakua wanaangalia sura ni kichapo tu bwenini hakubaki mtu tulikutana aubuh kila mmoja akitokea anakojua yeye.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…