Siku ya kwanza kuingia shule ya bweni ya Serikali

Daaaaaaah ningekua mimi ningemtimua jamaa siku hiyohyo nimalize mcheZo
 
Daaaaaaah ningekua mimi ningemtimua jamaa siku hiyohyo nimalize mcheZo
Nilikuwa mtu wa book, mkuu. Nilianza kupenda baada ya kumaliza university. Na book halikuniangusha kabisa. Sasa hivi hata serikali ya CCM ikiamua kutokutoa mafao kabisa, mtalia wenyewe bila mimi.
 
Kwamba ukamla afu ukampotezea au??
 
Miraji akumbukwe kwakweli, afande side na babu chacha sijui wako wapi nao!!!
lile bwawa la samaki limechimbwa Na wanafunzi,wahanga wa marehemu miraji.ile ofisi yake alikuwa anapaita Kandahar,hatoki mtu salama kule.
 
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Niliripoti shule siku ya jumapili, ilikuwa ni siku ya wali. Nikapokelewa mpaka bwenini na wenzangu, kwa kuwa ilikuwa ni muda wa msosi basi nkabeba messtin yangu huyo mpaka jikoni. Kufika kule nkakuta wageni wenzangu tukaambiwa leo nyie mtakula ugali na maharage wali mtaanza kula wiki ijayo.

Nikachukua chakula nilichopewa, nikaonja kidogo nikaona ladha hairidhishi pia kulikuwa na wadudu wanaogelea basi nikamwaga jalalani.
Kwa siku mbili mfululizo hali ikawa ile ile nashindwa kula na maji nannua ya chupa kwenye duka la shule. Siku ya tatu nikajisemea moyoni nitaishi kibishoo mpaka lini..?, nikafungua moyo nikaanza kuishi kikamanda na life likasonga freeeshi tu mpaka namaliza shule.
 
Dah mwenyekiti, kama kawaida yako!!
 
Ha ha ha haaaaaaa... Mwenyekiti ilifaa wewe ndio uwe mwenye huu uzi.. Omba hati miliki basi kwa mzee mama.
 
Ile nimefika tu form V pale mjini Tanga, nilifika kwa kuchelewa kama wiki 3. Nakuta watu wanasolve necta ya form VI tena maswali ya complex number wakati hata topic nilikuwa siijui inahusu nini. Nilipagawa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…