Siku ya kwanza kuingia shule ya bweni ya Serikali

Yaani nimecheka eti akawa anaiba hadi vile asivyo na kazi navyo anatupa, namuingiza rasmi kwa kamati ya roho mbaya.
Haha mbona walijua kumuonea mume wangu jamani mweeh. Naona akajifunza na "ujambawazi" kabisa, bora na yeye aibe
 
Yaani nimecheka eti akawa anaiba hadi vile asivyo na kazi navyo anatupa, namuingiza rasmi kwa kamati ya roho mbaya.
Yani nimewaza what if wanangu wakarithi roho mbaya from both parents, nimeishia kukemea
 
Hahahahahahhaahaah nimecheka Sana

Yaan wewe unawaita washamba na wameshakuibia
 
Tarime Secondary 2004.

Ilikuwa j3 ya wiki ya kufungua, hapo nimehama kutoka Mkolani Secondary kwa Mazula nikataka kwenda boardin nikapelekwa Tarime, picha linaanza nafika shule na Mama, nikapelekwa mpaka ofisini kwa second na bag langu kubwa na ndoo, sikununua fyekeo wala jembe. Ticha namshangaa anauliza mbona begi kubwa! Nikamwambia ni nguo za kubadili hizo nikaambiwa hizo za nyumbani hazihitajiki, zinahitajika mbili tu za kuvaa siku tukifunga, bi mkubwa akarudi nazo, mchana nikawa nimeshakula, ishu ikawa jioni, kwenda dining nakutana na wajomba wa form 5 na 4 na 6 na wengine hapo mimi niko form 3. Harage gumuuu, kuna jamaa alienipokea akanambia nisiogope, pale pako sawa, nikamwambia haina tabu. Harage likaungwa na mafuta mezani likatiwa pili pili ya kutosha watu tukaanza kupiga ugali. Badae prep huku baridi inanipiga hatari, baada ya siku ka 3 nikaona haya maisha hapa nitakufa, nikajitungia ugonjwa ili nirudi hom na ilikuwa nikirud ndio nitolee hapo, hamad! Baada kama siku mbili hivi mshua akaja shule akitokea Kenya akaja na mazaga kibao akaanza kuniusia hapo nisome, nikatulia. Maisha yakawa fresh tu, dining nikawa sikosi na pesa nilikuwa nayo nyingi tu ingawa sijuagi mpaka leo nilikuwa naitumia kwenye nini
 
Wakauchote wapi [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Umenikumbusha kitu wallah ,unaenda zako na kanga na toilet paper,ukishatoka ndio unaenda kuvaa nguo la sivyo unanuka choo nguo zote,, hivi kwanini jamani vyoo vile vilikuwa na nini
 
Huu uzi nausoma watu wananishangaa tu navyocheka..JF kwa tamu
 
Wewe Martial hater kumbe umesoma kiliboys mkuu pale...
 
Mimi nimesoma bagamoyo secondary, shule pekee ukiwa ufukwen au baharin unaogelea unakua bado upo eneo la shule, kama advance hukusoma serikalin bas ww ni kilaza
Asantee

Haya wewe uliyesoma serikalini advance vp uko wizara gani sasa hv mkuu

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Asantee

Haya wewe uliyesoma serikalini advance vp uko wizara gani sasa hv mkuu

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Nipo tamisemi Dodoma, na ww wa shule binafsi unaendeleaje na private sector hapo
 
Write your reply...nakumbuka kuvamia shamba LA shule kuchuma mkungu wa ndizi na kuuchoma bahat mbaya tukachoma shamba tulitoka nduki huku tukikimbizwa na mlinzi akijua waizi .bila kusahau nipo shule mwezi lakin sionekani darasani dining wala wapi route zangu ni Dom chaka na kitaa
 
I was luck, wakat naenda kuripot form five mzee alinisindikiza na gari ya ofisin kwake (STK) ile kufika tu shule sa 11 jion nikakuta wajomba wako parade basi nikasushwa pale kila mtu akaniona, ile STK ikamchanganya jamaa m1 akanipokea akanipeleka bweni moja la'kisure sana tulikua tunaliita UN (umoja wa mataifa), kiongoz wa chakula alikua anakaa UN ko tulikua tunakula na kusaza chakula daraja la kwanza. The following morning naamka nakuta wajomba wanaoga nje vimat*ko nje nje akat bafu zipo, with time na mim nikajikuta bingwa wa kuoga nje mixa kukatiza bweni to bweni na boxer tu [emoji28]! Nilijifunza mengi those days
 
Khe khe [emoji1787] khe [emoji1787] khe [emoji1787] khe khe [emoji1787] khe [emoji1787] khe [emoji1787]
 
Form 5 nilipangiwa na shosti angu tena comb moja..... Tukaenda wote tumevuuta hatari tumefika shule tunajikuta masista duu wajanja ndo sis asubuhi tunashangaa kuamka saa kumi na moja asubuhi hapo unapangiwa kufagia uwanja mkubwaa,afu umwagilie garden mpaka iwe tifu tifu baada ya hapo ukadeki choo afu saa moja sharp uwe parade ....aisee ikabid niulize hiz Kazi mpaka lini nikajibiwa ndo maisha ya kila siku niliangua kilio kisicho na mfano siku ya kwanza nikasema haya maisha siwez ,
Mda wa parade nipo na shati la tomato kidogo dogo na sketi ya kisista duu ya kiunoni nilikua nmeshashona home mwee mweee mwalimu kupita akatutoa mbele kwamba m shoga angu tumevaa kihuni tukapelekwa kwa Fundi wa shule tukashonewa mpaka shati kubwa kama la baba paroko kitamba kama cha shuka daa huku sket ya tumboni ndefu hatari
Nilienda na kikombe cha udongo kidogo dogo cheupe kama cha kahawa vile na kisahani changu kidogo kama kisosi maana o'level shule niliotoka full ubishoo ,doooh kufika SAA nne uji madai hatunywi tumbo litakua kubwa afu nashangaa watu wana majagi hahahaha..... Mwezi mrefu nikatafuta jagi langu na bakuli kubwa tu tena la plastic uji nikaunywa vizuri tuuuu na foleni ya ugali nikapanga
Shule ilikuwa kanda ya ziwa washamba washamba wengi tukaanza kuwacheka wahaya kwamba mjini wanajishauaga saana ila kumbe wana lafudhi mbovu inshort ni wakuja tuu tuliwacheka saana....

Nakumbuka siku ya kwanza tu nilipiga simu nyumban maisha magum siwez mzee akanimbia vumilia mpaka muhula uishe ndo utahama ,sasa muhula daah Kazi nying afu viongoz walikua wanaishi kwa raha saana hawafanyi kazi yeyote nikaona bora nikimbilie uongoz bahati mbaya viongoz wote form6 na uchaguz mpaka muhula wa pili ,siku ya kufunga niliondoka na kila kitu changu kufika nyumban shule nilizotaka kuhamia background ya result zao kwa comb yangu sio nzur tena wasichana ndo kabisa div3 , div4 na 0 maana nilikua pcm nikasema hapana bora nilipotoka comb yangu wanafaulu nikarudi baada ya miez miwili na tranka langu hahahaha nikakuta mwalimu wa zamu mnoko hatari akanipa adhabu ya kuvuta akanikatia shamba la kulima na kuchimba na kuzisombelea molam ndoo 25 ,shamba nikaajiri wanakijiji kimbembe molam anasimami nikabeba kufika ndoo ya 10 viungo vya mwili vikagoma havina ushirikiano kabisa naumwa kila sehemu nalia hatari nikarud Dom nikampigia mzee nikamwambia akasema nipe namba za mwalimu wako nikampa sijui waliongea nin baadae nashangaa naitwa sikwenda mwl akaja nipo kama nakaribia kufa akaniambia adhabu umesamehewa

Muhula wa pili baada ya mda ikafika kipind cha uchaguz nikasema hapa lazima niwe kiongoz kwa mikaz ya shule naweza kufeli bure nikachukua fomu bahati nzur kichwani nilikua vizuri nikachaguliwa academic
Baada ya kuwa kiongoz ndo maisha yakaanza sasa kwanza nikachagua room nayotaka ,ambazo nitofaut na wanafunz wa kawaida ndani mnakaa wawil tu chumba mapazia ,carpet hapo ndo nikaish kama nipo chuo mpaka namaliza .....

Nashukuru tu Mungu nilifaulu vzuri
 
Pole sana mkuu

Mi mzee wangu alikua ananipenda sana ... !!!

Shida nilizopitia ni yale ma quantum phyz
 
Aisee pole sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…