Inaniuma sana (From the audio, not official lyrics)
Siku ya kwanza kukutana nae alikuja kwetu usiku,
Alikuta nimechoka nimetoka kurekodi usiku,
Walikuwa kama wanne hivi ndani ya gari aina ya chaser,
Wamejaa hangover utadhania jana yake walikesha,
Akaja mshikaji wangu mmoja, kutoka kwenye ileile gari,
Akaja moja kwa moja, mpaka kwenye mlango wa geto,
Nature..Nature.. kuna mtu anakuhitaji embu toka umuone,
Ku kutoka nje namkuta msichana nnayemfahamu kwa jina la Tina, ambaye alisoma DSJ chuo kile kikuu cha habari,
Na na katika kipindi hichi chote alikuwa anaishi hostel,
Mshkaji akamuita, akasema huyo mchumba huyu hapa,
Njoo uchonge nae..muelewane..twende tukajichane..
Inaniuma sana, nikifikiria, huwaga mi nalia..
Inaniuma sana, vina za kufanya, vinakosekana..
Inaniuma sana, hata watoto wadogo wananicheka sana.
Inaniuma sana, nikifikiria, huwaga mi nalia..
Inaniuma sana, vina za kufanya, vinakosekana..
Inaniuma sana, demu wangu amepima amekutwa ana ngoma.
Mambo?!!.. safi tu aunt, sijui una matatizo gani..
Akang’ata vidole, ili nimuone bonge la shori,
Sikujua alichotaka, ila niliona ni miujiza,
Mtoto mdogo wa kike kunifata usiku uliojaa giza,
Kuanzia juu mpaka chini shepu yake ni ya kuigiza,
Aunt si ushaniona, mi naondoka naenda zangu kulala,
Na isitoshe usiku sahizi dingi akiskia ni msala,
Akang’ata vidole, akaangaliana na wenzake, halafu wakapeana kama ishara (hihihi😆😆)
Kama kuna mademu kama hawa, asilimia tisini watakuwa wanaugua miwaya,
Hii singo inalizwa hailizwi hivihivi, nikikumbuka kipigo ambacho anapigwa mwizi, kinachofatia ni kifo hata kama awe ana hirizi,
Narudia topic hii, samahani washkaji kwa usumbufu, kwa kusikiliza maneno matamu yenye ubunifu,
Akarudi msichana akiwa na huzuni tokea jana,
Naomba kampani yako twende tukatese bilicanas,
Okay, hamna shaka twende tukafanye unachotaka..
Inaniuma sana, nikifikiria, huwaga mi nalia..
Inaniuma sana, vina za kufanya, vinakosekana..
Inaniuma sana, hata watoto wadogo wananicheka sana.
Inaniuma sana, nikifikiria, huwaga mi nalia..
Inaniuma sana, vina za kufanya, vinakosekana..
Inaniuma sana, demu wangu amepima amekutwa ana ngoma.
Uuu unadai unakwenda shooting, kumbee.. ii unakwenda kufanya booking,
Mbona hujitangazi kuwa hivi sasa bwana wewe unauza,
Ili kuwasevu washkaji wao wapate nao kujiuguza,
Wee bwana, hebu angalia huo uthamani waa wa utu wako,
Halafu tofautisha na uthamani huo wa upumbavu wako,
Kwa kucheza dili, na magazeti, huwezi kuharibu jina,
Haya suala, hili suala kubwa ni lako mama usimsingizie Nina,
Endelea kuponda mali mtoto, Mungu wetu atakusaidia,
Kila akitoka tuu, mpenzi wangu muandike umeumia,
Wanaume wapo wengi, wanene na wenye fedha fedha nyingi,
Ambao wanapenda mademu kama nyinyi wenye wanaume wengi,
Wenye nguvu za simba, na wasioogopa risasi,
Na wenye kuhonga twelve million or six dollars..
Inaniuma sana, nikifikiria, huwaga mi nalia..
Inaniuma sana, vina za kufanya, vinakosekana..
Inaniuma sana, hata watoto wadogo wananicheka sana.
Inaniuma sana, nikifikiria, huwaga mi nalia..
Inaniuma sana, vina za kufanya, vinakosekana..
Inaniuma sana, demu wangu amepima amekutwa ana ngoma.
Huu ni mtambo wa kurekebisha tabia, umeskia..
Wa kwanza alikuwa dereva taxi, imevuma tetesi,
Wa pili alikuwa mwenye pickup, akachangamkia chapchap, nilihuzunika sana hii kitu mimi sitosahauu,
Ulipigwa denda mpaka gari ikagoma kwenda,
(………..??hapa kiroboto kaniponyoka), starehe kupeana milenda, kabla ya kuondoka uliniomba hela ya kwenda,
Ukaniambia nisiwe na hofu mimi niko peke yangu,
Siri ikafichuka, mlipotoka mlipokwenda,
Kuna mlevi mmoja alilewa akaropoka,
Huko tulikokwenda mshkaji wangu noma kweli 😆,
Sita na mwenye gari mmoja si walinyonyanaa, ndimi nje nje..
Hadi kupata ajali wakati mumewe yu safari,
Nikikuuliza, aah aah bwana we, wana wivu hao..
We binadamu gani uchukiwe na kila mtu bwana,
Au kwa kuwa mrembo mfupi na mzuri sana,
Hao ni baadhi tu ambao mimi nafahamu mimi,
Wengine ni rafiki zangu nikiwataja huwezi kuamini,
Haya wewe si msanii, nenda kalipize kwenye tv…