matunduizi
JF-Expert Member
- Aug 20, 2018
- 7,968
- 19,368
Unaweza kushangaa lakni siku ya kwanza kula tikiti maji ilikuwa mwaka 2003.
Nilikuwa napita sokoni tu ila sijui ni nini.
Ni kama upite mitaa ya wahindi utakutana na mboga za majani ma matunda ambayo tangu mama muuza genge mtaani kwenu afungue ujasiliamali wake miaka 50 iliyopita hajawahi kuyauza.
Niliingia sokoni nikanunua kipande. Ule wekundu nilikuwa najua ni mchachu kama limao hivi.
Kwa Kuogopa aibu nikalitila mfukoni, nikapanda daladala na kutokomea kunakojulikana kando ya mlima flani ili nilile tunda lile kitafiti zaidi hata likinishinda nilitupe.
Tangu siku ile kwa utamu ule, na utafunwaje wake unaopukutika kama unakula biskuti flani tuliziita '' wafer'' niliburudika sana na kulifanya kuwa tunda langu bora la muda wote hadi naingia kaburini.
Ukisikia ninaumwa niletee tikiti maji, hata kama niko mahututi nitajitahidi angalau nililambe tu.
Matunda mengine niliyala kwa mara ya kwanza ukubwani ni.....
1: Tufaa / Apple
2: Fenesi
3: Yale matunda mekundumekundu wanasema ndio maembe ya iringa.
Hebu toa uzoefu wako, Kuficha ukweli wako kwenye mambo madogomadogo kama haya ni ujinga sio ujanja.