Siku ya Kwanza Kula tikiti maji

Siku ya Kwanza Kula tikiti maji

matunduizi

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2018
Posts
7,968
Reaction score
19,368
Unaweza kushangaa lakni siku ya kwanza kula tikiti maji ilikuwa mwaka 2003.
Nilikuwa napita sokoni tu ila sijui ni nini.
Ni kama upite mitaa ya wahindi utakutana na mboga za majani ma matunda ambayo tangu mama muuza genge mtaani kwenu afungue ujasiliamali wake miaka 50 iliyopita hajawahi kuyauza.

Niliingia sokoni nikanunua kipande. Ule wekundu nilikuwa najua ni mchachu kama limao hivi.
Kwa Kuogopa aibu nikalitila mfukoni, nikapanda daladala na kutokomea kunakojulikana kando ya mlima flani ili nilile tunda lile kitafiti zaidi hata likinishinda nilitupe.

Tangu siku ile kwa utamu ule, na utafunwaje wake unaopukutika kama unakula biskuti flani tuliziita '' wafer'' niliburudika sana na kulifanya kuwa tunda langu bora la muda wote hadi naingia kaburini.
Ukisikia ninaumwa niletee tikiti maji, hata kama niko mahututi nitajitahidi angalau nililambe tu.

Matunda mengine niliyala kwa mara ya kwanza ukubwani ni.....

1: Tufaa / Apple
2: Fenesi
3: Yale matunda mekundumekundu wanasema ndio maembe ya iringa.

Hebu toa uzoefu wako, Kuficha ukweli wako kwenye mambo madogomadogo kama haya ni ujinga sio ujanja.
 
Juzi hapa nilimlazimisha rafiki yangu kula parachichi. Alikuwa hajawahi kula kabla ya hapo. Sasa kila nikimshawishi alikuwa hataki. Nikakata kipande kidogo hivi cha pembe tatu.

Nikamwambia kula hata hucbi kidogo huku usilifikirie, jamaa akala.

Aiseeh. Unajua alisemaje

"Kuna kipande chengine hapo uniongeze".

Sent using Jamii Forums mobile app
 
duu,
mkuu mimi nimeshangaa eti parachichi watu wanalia hadi ugali na wali.
wakati home enzi hizo yalikuwepo yakiiva tunayachezea tu tulipokuwa watoto.
Hilo naliona tangu mdogo ila nikionja tu nahisi kutapika. Juzijuzi baada ya kugundua ni la Muhimu nikaanza kunywa sharubati (Juice yake) Sikuhizi na mimi nimeiga kula japo kwa kujilazimisha.

Mimi nilizoea, Stafeli, maembe dodo, topetope, maembe madogo, sungwi.
Jamaa nikiwashangaa wanapendea nini parachichi wananicheka.
 
Tikiti Tikiti maji au Tikiti nini? Ukaenda kulilia wapi vile? Kwanini sio nyumbani?

Sent using Jamii Forums mobile app
Tikiti maji mkuu kwani kunatikiti barafu.
Nilienda chobisi makusudi ili nipate uzoefu nikiwa peke yangu, nilikuwa mwanafunzi enzi hizo so ningegundua ni zuri nilipanga nirudi kwa vijana wa mtaani niwashawishi niwe kama expert wake, na adhma ilitilima maana wengi waliokuwa hawayali kutokana na rangi ya ubichi ( enzi hizo yalikuwa yale ya kijani kibichi) tulikuwa tunayafananisha na matunda flani porini ambayo tuliaminishana ni matunda yenye sumu.

Tuliamini Tunda lililoiva lazima litoke kwenye ukijani kwenda rangi nyingine, Sasa Tikiti muda wote ni la kijani, nilikuwa nikiliona meno yanakufa ganzi nikijua ni chachu balaa.
 
duu,
mkuu mimi nimeshangaa eti parachichi watu wanalia hadi ugali na wali.
wakati home enzi hizo yalikuwepo yakiiva tunayachezea tu tulipokuwa watoto.
Hilo naliona tangu mdogo ila nikionja tu nahisi kutapika. Juzijuzi baada ya kugundua ni la Muhimu nikaanza kunya sharubati (Juice yake) Sikuhizi na mimi nimeiga kula japo kwa kujilazimisha.

Mimi nilizoea, Stafeli, maembe dodo, topetope, maembe madogo, sungwi.
Jamaa nikiwashangaa wanapendea nini parachichi wananicheka.
Kama. Hauli.parachichi basi ujue unakosa vitu vingi. Sana ktk mwili. Wako yaani. Yanafaida kwa. Afya hakuna tunda linasogea hata kidogo

{Hutajuta ukitembelea
& kusubscribe chanel yangu ya youtube jina Misifa Skills,Link hii hapa
 
'Topetope' hili tunda nimeliona na kufanikiwa kulila wiki 3 nyuma, iliniwia vigumu kidogo, maana lina maji na sukari kama yote, halafu ni tepetepe sana.
Hilo topetope ni tunda gani mbona silijui aisee naomba picha yake tafadhali

{Hutajuta ukitembelea
& kusubscribe chanel yangu ya youtube jina Misifa Skills,Link hii hapa
 
Kama. Hauli.parachichi basi ujue unakosa vitu vingi. Sana ktk mwili. Wako yaani. Yanafaida kwa. Afya hakuna tunda linasogea hata kidogo

{Hutajuta ukitembelea
& kusubscribe chanel yangu ya youtube jina Misifa Skills,Link hii hapa

sawa mkuu
 
'Topetope' hili tunda nimeliona na kufanikiwa kulila wiki 3 nyuma, iliniwia vigumu kidogo, maana lina maji na sukari kama yote, halafu ni tepetepe sana.
ukibaatisha topetope lililoiva vizuri, ni tamu mnoo
 
Kuna tunda linaitwa kiwi... Natamani siku nlionje.. But hisia zangu zinaniambia lina ladha mbaya kuliko matunda yote

Sent using Jamii Forums mobile app
hili huwa naliona kwenye mavitabu ya kizungu tu, siku nikiliona lazima nilionje pia. Haiwezekani mwaka mzima unakula matunda aina nne au tano tu, labda ndio maana akili zinakuwa za kuungaunga.
 
Kuna mzee mmoja Dodoma aliniambia kama una homa ya ndani ambayo haijajitokeza ukila tikiti maji lazima homa ipande. Nami nilijaribu ilikuwa miaka ya mwishoni ya tisini ndio mara yangu ya kwanza kula nilipata mpaka yellow fever.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna tunda linaitwa Pama lipo kama Nazi lakini lenyewe lipo sana kanda ya kati shy ,tbr,SGD sijawahi kulielewa kabsa lakni naona watu walitafuna kwelikweli
 
Kuna tunda linaitwa Pama lipo kama Nazi lakini lenyewe lipo sana kanda ya kati shy ,tbr,SGD sijawahi kulielewa kabsa lakni naona watu walitafuna kwelikweli
da hili silijui au ndio lile la kwenye miti flani kama mnazi kula wanaiita mihama, ndio chanzo cha neno kahama?
 
Kuna mzee mmoja Dodoma aliniambia kama una homa ya ndani ambayo haijajitokeza ukila tikiti maji lazima homa ipande. Nami nilijaribu ilikuwa miaka ya mwishoni ya tisini ndio mara yangu ya kwanza kula nilipata mpaka yellow fever.

Sent using Jamii Forums mobile app
mkuu mimi baada ya kuanzisha mahaba na tikiti, ninaweza kushindwa kula vyote ila sio tikitimaji. na nikila hata hamu ya kula vingine inaongezeka. Hiyo ya Homa ntajaribu siku nikiona homa inanivizia.
 
Tikiti maji mkuu kwani kunatikiti barafu.
Nilienda chobisi makusudi ili nipate uzoefu nikiwa peke yangu, nilikuwa mwanafunzi enzi hizo so ningegundua ni zuri nilipanga nirudi kwa vijana wa mtaani niwashawishi niwe kama expert wake, na adhma ilitilima maana wengi waliokuwa hawayali kutokana na rangi ya ubichi ( enzi hizo yalikuwa yale ya kijani kibichi) tulikuwa tunayafananisha na matunda flani porini ambayo tuliaminishana ni matunda yenye sumu.

Tuliamini Tunda lililoiva lazima litoke kwenye ukijani kwenda rangi nyingine, Sasa Tikiti muda wote ni la kijani, nilikuwa nikiliona meno yanakufa ganzi nikijua ni chachu balaa.
Tikiti barafu 🤣🤣🤣

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom